![]() |
A burnt-out
car hangs precariously over the edge of the collapsed structure.
|
![]() |
All floors
of the car park were affected.
|
![]() |
The top
floor of the car park led into the Westgate mall.
|
![]() |
As dawn
broke over the Westgate mall, smoke still rose from behind the main complex.
|
Gazeti la
New York Times la Marekani lilikariri vyanzo vyake ndani ya vyombo vya usalama
vya nchi hiyo jana vilivyosema kuwa mipango na mazoezi kwa ajili ya shambulizi
hilo vilifanyika Somalia.
Magaidi kati
ya 10 hadi 15 wa Al-Shabaab walivamia kwa silaha kwenye jengo la ghorofa nne la
maduka na kusababisha vifo vya watu 76 kwa mujibu wa taarifa za Serikali ya
Kenya na majeruhi 175 huku Magaidi watano walipoteza maisha kwenye tukio hilo
na wengine 11 kukamatwa.
Kitengo cha
Mambo ya Nje cha Kundi la Al-Shabaab ndicho kilichokuwa na kazi ya kupanga
shambulizi hilo.
Imeelezwa
kuwa watekelezaji wa tukio la kigaidi walipitia mafunzo maalumu huko Somalia
yaliyowawezesha kubaini michoro ya jengo pamoja na mbinu za kusafirisha silaha.
Utekelezaji
Gazeti hilo
lilidai kuwa uratibu wa operesheni hiyo ulifanywa kwa uangalifu kwani wafuasi
wa Al-Shabaab waliochaguliwa ni wale ambao walikuwa wanafahamu vyema Kiingereza
na wenye uzoefu wa masuala ya kimataifa.
“Hawa jamaa
pia waliandaa mchoro wa jengo hilo. Wakaandaa mkakati wa kupenyeza silaha
ambazo walikuwa wamezileta kutoka Somalia,” kilisema chanzo cha gazeti hilo.
Gazeti la
New York Times, lilisema silaha zilizotumika kwenye uvamizi huo zilipenyezwa
kupitia maeneo yalikuwa yakilindwa na askari wa kampuni binafsi za ulinzi.
Duru za
usalama za Marekani zimeeleza kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa baadhi ya askari
walihongwa kutokana na kukabiliwa na ukata wa kutolipwa kwa wakati na waajiri
wao.
Taarifa
zinasema kuwa siku moja au mbili kabla ya uvamizi huo, inasemekana magaidi hao
walipitisha kwa siri mikanda ya risasi kwa ajili ya kutumika kwenye bunduki zao
aina ya `Short Machine Gun’ (SMG).
Baadhi ya
wafanyakazi wa jengo hilo wanadaiwa kula njama na magaidi hao ili kufanikisha
mpango wa kuingizwa kwa silaha hizo zilizotumika kwenye ugaidi.
Taarifa
zaidi zinasema kuwa mmoja wa magaidi hao alikuwa amebeba nguo za kubadilisha
ambazo angezitumia na wenzake kwa ajili ya kutoka nje ya jengo hilo pamoja na
raia wakati wa kukimbia baada ya kufanya mauaji.
Serikali ya Kenya imetoa
orodha ya washukiwa wa shambulizi hilo wanaotoka Marekani na Uingereza.
Rais Uhuru
Kenyatta alisema taarifa za kiusalama zimedokeza kuwa mashambulizi hayo
yalitekelezwa na raia watatu kutoka Marekani na mwanamke mmoja wa Uingereza.
Wizara ya
Ulinzi ya Marekani imesema imepokea taarifa za kuhusika kwa raia wake, lakini
imesisitiza kuwa bado haiwezi kudhibitisha moja kwa moja mpaka pale itakapopata
uhakika kwa njia ya vipimo vya kinasaba (DNA).
“Tunafahamu
yaliyotokea Kenya, lakini hatuwezi kuthibitisha moja kwa moja kuhusika kwa raia
wa Marekani, tunasubiri vipimo vya DNA pamoja na baadhi ya picha za kwenye
mitambo ya CCTV... lakini tendo lililofanyika nchini Kenya ni la kinyama,”
alisema ofisa mmoja wa usalama wa Marekani ambaye hakutaka jina lake kutajwa
alipohojiwa na New York Times.
Serikali ya
Kenya imesema imedhibiti eneo zima la jengo na kuwaua baadhi ya magaidi hao
ingawa nchi za Ulaya na Marekani zinaona kwamba kuna uwezekano baadhi ya
wavamizi walifanikiwa kutoroka wakati wa kurushiana risasi.














No comments:
Post a Comment