![]() |
|
Baadhi ya wananchi waliokwenda kuionesha
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngara eneo la tukio katika kitongoji cha Ngoma kijiji cha Kasulo.
|
![]() |
|
Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngara ikijianda kuondoka eneo la tukio.
|
Seikali ya kijiji cha Kasulo
wilayani Ngara mkoani Kagera imekanusha
taarifa zilizotolewa na baadhi ya Wananchi kupitia baadhi ya vyombo vya
habari kuwa kuna mauaji ya watu wawili
yaliyotokea Kijiji humo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kasulo
wilayani Ngara Bw.Yusufu Katula alisema hayo jana(Septemba 26,2013) wakati
akiongea na Wananchi wa kitongoji cha Ngoma kilichomo kijijini humo alipoambatana na kamati ya ulinzi na usalama
ya wilaya ya Ngara.
Bw.Katula alisema mauaji
yaliyofanyika kijiji humo yaliandaliwa
na waharifu wanaojiita wanaharakati
ambapo wananchi na viongozi kwa
kushirikiana na vyombo vya dola wanawasaka ili kuwafikisha kwenye mkondo wa
sheria.
Alisema mhamasishaji wa mauaji ambaye
alitoroka Bahati Gervas ndiye kichochezi akitafuta umaarufu wa kuwaondoa
wahamiaji wenye mifugo eneo la Ngoma licha ya kutokuwa na mchango wa maendeleo
kijijini humo.
“Mauaji hayo hayahusiani na mmoja wa
wafugaji Athumani Makoye kwani huyo ni
mwananchi halali na mpenda maendeleo
maana ametumia fedha nyingi kujenga shule ya kitongoji hiki”…Alisema Katula.
Mauaji hayo yaliyofanyika Septemba 19 ,Mwaka
huu yalihusisha kukatwa katwa kwa ng’ombe 15 wenye thamani ya Shilingi Milioni
8.4 mali ya raia wa Rwanda kwa kile kilichoelezwa awali kuwa ni vurugu baina ya
wakulima na wafugaji.
Hata hivyo Mwenyekiti wa kamati ya
ulinzi na usalama ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw.Costantine Kanyasu
aliwataka wananchi wa kijiji hicho
kuacha kijichukulia sheria mkononi na kusababisha maafa katika kijiji chao.
Bw.Kanyasu alisema serikali kwa kushirikiana
na wananchi wazalendo tayari wameanza kuwakamata waliohamasisha mauaji na kwamba hata waliokimbia na kutoroka
watawasakwa ili wafikishwe Mahakamani
kujibu tuhuma zinazowakabili.
Habari/Picha Na:-Shaaban Ndyamukama.












No comments:
Post a Comment