Watuhumiwa tisa
wa kesi ya wizi wa mafuta katika mgodi wa Dhahabu( GEITA GOLD MINE ) kwa kutumia
gari la wagonjwa (Ambulance) wamefikishwa katika Mahakamani ya wilaya ya Geita na
kusomewa mashitaka matatu yanayowakabili.
Mwendesha
mashitaka wa polisi Inspekta Abiner ameiambia mahakama kuwa mnamo 05/09/2013 saa 7:30 usiku uko eneo
la Geita Power ndani ya mgodi wa Geita Gold Mine watuhumiwa waliiba mafuta lita
630 ya dizeli, kula njama za kuiba mafuta hayo ,kuaribu mali ambayo ni gari la
kubeba wagojwa katika kituo cha Afya cha Nzera kwakuling’oa viti.
Mwendesha
mashitaka amedai kuwa mtuhumiwa wa kwanza Hamudi Biemo (28) Dereva wa gari hiyo
anatuhumiwa kwa makosa matatu likiwemo la kula njama na kung’oa viti vya gari
hilo kwa lengo la kubeba mafuta hayo.
Mwendesha
mashitaka huyo ameendelea kuiambia mahakama kuwa watuhumiwa 8 wanakabiliwa na
makosa 2 ,Wizi wa mafuta na kula njama ya kuiba mafuta hayo.
Abiner
ameongeza kuwa washitakiwa hao walitumia gari aina ya Land Crusser yenye namba
za usajili T 671 AKW ,Mali ya Halmashauri ya wilaya ya Geita nakuingia mgodini nakuiba mafuta aina ya
Diesel lita 630 zenye thamani ya Shilingi 1,386,000/= mali ya Mgodi wa Dhahabu
wa Geita (GGM) .
Waliofikishwa
mahakamani ni Hamudi Biembo dereva wa gari la wagonjwa ,Malemo Paul (31) mkazi wa mtaa wa Mseto Geita,Selemani Magoso (31 )ambaye ni
dereva pikipiki mkazi wa mtaa wa Shilabela Geita, Julias Boazi (28) mkazi wa
Msalala road Geita ).
Wengine ni
Rashid Hussen (27) Mlizi wa mgodi, Ismail Zuber (26)mlinzi wa Kampuni ya G4S
,Christoper Kombo Operator wa GGM,Joseph Chiristopher (27) Operator wa GGM.
Aidha Wasitakiwa
wote (9) wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti na kesi yao bado inaendelea kusikilizwa katika Mahakama ya
wilaya ya Geita.
Habari/Picha
Na:-Denice Stephano.



















No comments:
Post a Comment