![]() |
Baada ya
sakata la kuibiana nyimbo lilichokua takribani siku mbili kati ya msanii
Diamond Platnum na Dayna Nyange,producer Shedy ameamua kukata mzizi wa fitina
kwa kuuanika ukweli wa mambo.
|
Akiongea na
#Team Tz,Shedy amefunguka kama ifuatavyo:-
“Beat hii
nilitengeneza mimi kwa idea zangu mwenyewe. Alikuja Dayna akaupenda ule mdundo
na mimi sikumnyima , akafanya demo lakini hakulipia kitu.
"Sasa
ikapita zaidi ya miezi sita kila nikimuliza vipi anasema bado atakuja
kufanya.Kuna siku Diamond akaja studio ,akataka kusikia midumdo niliyonayo.
"Bila
hiyana, nilimchezea midundo mbalimbali kama mteja, ila jamaa akavutiwa sana na
ule mdundo ambao Dayna aliufanyia demo.
"Baada
ya Diamond kuupenda mdundo huo, niliamua kumpigia simu Dayna na kumuelezea
kwamba Diamond kapenda kufanya kazi katika ile beat,Dayna akakubali kabisa,
"Sasa
nashangaa yeye kusema diamond kamuibia wakati alikubali yeye mwenyewe."






No comments:
Post a Comment