Msemaji
wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Erick Komba akiongea na
waandishi wa habari leo katika ukumbi wa
mikutano uliopo makao makuu ya Jeshi hilo
jijini Dar es Salaam kuhusu ushiriki wa Tanzania katika operesheni ya
ulinzi na amani katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Tanzania
ni moja kati ya nchi tatu zilizopeleka kikosi chake nchini DRC ikiwa ni sehemu ya
SADC standby brigade inayotoa mchango wake katika Jeshi la Umoja wa Mataifa
(MONUSCO) na kinafanya kazi chini ya Force Commander huku majukumu yake yakiwa ni kuzuia waasi
kujitanua, kuvunja nguvu ya waasi na kuwapokonya silaha makundi yote ya waasi.
Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) Assah Mwambene.
Ushiriki wa Tanzania katika Operesheni ya
Ulinzi wa Amani nchini DRC, unatokana na mgogoro kati ya Serikali DRC na waasi
hususan kikundi cha waasi cha M23. Mgogoro huo ulianza mwezi Aprili 2012 ambapo
kikundi cha M23 kilijitoa katika Jeshji la serikali ya DRC na kuanzisha
mapigano hali iliyopelekea hali ya usalama nchini DRC kuwa mbaya.
Kufuatia
hali hiyo mbaya ya usalama, wakati wa kikao cha International Conference on the
Great Lakes Region kilichofanyika tarehe 12 Julai 2012 mjini Addis Ababa,
Ethiopia, Mhe. Rais Joseph Kabila aliwasilisha ombi kwa Wakuu wa Nchi za Maziwa
Makuu ambazo Rwanda, Uganda, Tanzania,
na DRC akaomba nchi wanachama wa Maziwa Makuu zisaidie kuwapokonya
silaha waasi wa M23.
Wakuu
wa nchi za Maziwa Makuu walikubaliana na ombi hilo na kutoa maelekezo kwa
Mawaziri wa Ulinzi ambao walikutana tarehe 01 hadi 2 Agosti 2012 na kujadili maelekezo ya Wakuu wa nchi za
Maziwa Makuu.
Mawaziri wa Ulinzi walikubaliana kuwa ni muhimu kwa vikundi vyote
vya Waasi (ADF, FDLR na M23) kushughulikiwa na wakawasilisha mapendekezo yao
kwa Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu.
Tarehe
7 Agosti 2012, Wakuu wa nchi za Maziwa Makuu walikutana tena mjini Kampala,
Uganda na kupanga mkakati wa kuanzishwa kwa ‘Neutral Intervention Force (NIF)’
na nchi wanachama wa Nchi za Maziwa Makuu zikaombwa kuchangia askari
watakaounda ‘Neutral Intervention Force (NIF)’ ambapo Tanzania iliombwa na
ikahadi kuchangia kikosi kimoja.
Kikao hiki kilitoa maelekezo ya hatua
inayofuata kwa Mawaziri wa Ulinzi wa Maziwa Makuu.
Tarehe
7 hadi 8 Sep 2012, Mawaziri wa Ulinzi wa maziwa Makuu, walikutana na kujadili
utekelezaji wa uanzishwaji wa ‘Neutral Intervention Force (NIF)’.
Wakaunda
‘Military Assessment Team (MAT)’ kufanya tathmini ya tishio.
Timu hiyo
ililifanya tathmini na kuwasilisha taarifa yake kwenye kikao cha Mawaziri wa
Ulinzi kilichofanyika tarehe 25 Oktoba 2012 mjini Goma, DRC na baadaye taarifa
hiyo iliwasilishwa kwa Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu ambao waliagiza
kushirikishwa kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika
(SADC), Umoja wa Afrika(AU) na Umja wa Mataifa(UN) ili kufanikisha mkakati huo.
Nchi
wanachamma wa SADC na Nchi za Maziwa Mkuu kwa pamoja walikubaliana na
kupendekeza SADC Standby Brigade ipelekwe DRC kama ‘Neutral Intervention Force
(NIF)’.
Kufuatia ridhaa hiyo nchi wanachama wa SADC ziliombwa kuchangia ambapo
nchi mbalimbali wanachama zilikubali kuchangia, lakini Umoja wa Mataifa(UN)
ilizipitisha nchi za Tanzania, Afrika Kusini na Malawi kuchangia askari nguvu
ya Brigedi moja kuunda NIF ya MONUSCO.
Aidha,
Umoja wa Mataifa mwezi Januari 2013 uliridhia mapendekezo ya Wakuu wa Nchi za
Maziwa Makuu na Nchi wanachama wa SADC ya kuundwa ‘Neutral Intervention Force
(NIF)’ na kupelekwa DRC.
Kufuatia idhini hiyo tarehe 28 Machi 2013, Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha
Azimio (Resolution) namba 2098 (2013) na kutoa jukumu maalumu la ulinzi
wa amani nchini DRC, likijumuisha ushiriki wa Neutral Intervention Force (NIF)
kama sehemu ya MONUSCO, na ikaitwa ‘Force Intervention Brigade (FIB)’ ambayo
kikosi cha Tanzania ni sehemu ya Brigade hiyo.
Kwa
mantiki hiyo ieleweke kwamba, Kikosi cha Tanzania kilichopo DRC ni sehemu ya
SADC standby brigade iliyotoa mchango wake katika Jeshi la Umoja wa Mataifa
(MONUSCO).
Kinafanya kazi chini ya Force Commander, MONUSCO na majukumu yake
ni:
Kuzuia
waasi kujitanua (Prevention of Expansion)
Kuvunja
nguvu za waasi (Neutralization)
Kuwapokonya
silaha makundi yote ya waasi.
Kwa
kuzingatia kuwa kikosi chetu kiko chini ya majeshi ya Umoja wa Mataifa ya
MONUSCO, inamanisha kuwa Operesheni hiyo ni ya Umoja wa Mataifa, Tanzania haipigani na M-23 na haina tatizo na
Rwanda kuhusiana na Operesheni hiyo na ridhaa ya kikosi chetu kwenda DRC
ilikubaliwa pia na Rwanda, nchi ambayo ni mwanachama wa nchi za Maziwa Makuu.
Aidha, Rwanda imesaidia sana kwa kuruhusu kikosi cha Tanzania kupitisha watu,
vifaa na zana katika nchi yake kupeleka DRC.






No comments:
Post a Comment