Mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kuhusu kongamano la uwekezaji litakalofanyika mwezi wa 10 mkoani humo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, September 06, 2013

Mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kuhusu kongamano la uwekezaji litakalofanyika mwezi wa 10 mkoani humo.

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Luteni kanali Mstaafu Issa Machibya akiongea na waandishi wa habari Jana (Septemba 05,2013)  katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam kuhusu kongamano la uwekezaji litakalofanyika mwezi wa 10,mwaka huu mkoani humo na kujumuisha wadau mbalimbali nchini, mabalozi wa nchi za nje, wafanyabiashara wa nchi jirani na Taasisi.


Kulia ni Abdulhakimu Ally mtaalamu wa mifumo ya Kompyuta akifuatiwa na George Busungu ambaye ni katibu tawala msaidizi mipango la uratibu wa mkoa huo.

Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Kigoma Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya (hayupo pichani ) wakati akiongea nao kuhusu kongamano la uwekezaji litakalofanyika mwezi wa 10 mkoani humona kujumuisha wadau mbalimbali nchini, mabalozi wa nchi za nje, wafanyabiashara wa nchi jirani na Taasisi. Mkutano huo umefanyika leo katika ukumbi wa mikutano uliopo Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam.

Picha na Anna Nkinda – Maelezo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad