Katibu wa
NEC ya CCM itikadi na Uenezi amesema kinachowasumbua Chadema mpaka wanafanya
yote waliyoyafanya hasa ngumi na vurugu bungeni ni namna watakavyoeleza kwa
waliowapa pesa za kuvuruga mchakato wa katiba nchini kwani wanatakiwa kupeleka
mrejesho jinsi walivyofanikiwa na jinsi walivyotumia mabilioni hayo.
Nape
ameyasema hayo kwenye mkutano mkubwa wa hadhara mjini Kahama kwenye ziara ya
karibu siku ishirini kanda ya ziwa kwa mikoa mitatu yaani Shinyanga,Simiyu na
Mara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndg. Abralhaman Kinana.
"Wenzetu
hawa nasikia wamepewa mabilioni toka nje kwa kisingizio cha kushiriki mchakato
wa katiba, na kama ilivyo kwa vibaraka wengine katika bara la Afrika lengo la
mapesa hayo sio kuwawezesha kushiriki bali kuanzisha fujo na vurugu ili
mchakato usimalizike salama iwe ajenda 2015 kwani kimsingi hawana ajenda
mpya" alisisitiza Nape.
Akielezea
swala la pesa kutoka nje Nape alisema mara tu baada ya rasimu ya kwanza kutoka
Katibu Mkuu wa Chadema alikwenda nje ya nchi na akakaa kwa muda na aliporudi
tu, ndio Chadema wakapanga kuanza kuzunguka na helkopta.
"Babu
atwambie alifuata nini nje? Na pesa za kuzunguka na misafara miwili tofauti ya
helkopta walitoa wapi? Na watwambie kama walisharudisha mrejesho kwa wafadhili
wao" alisema Nape.
Nape
aliendelea kusisitiza kuwa yote yaliyotokea bungeni si mambo yaliyotokea kwa
bahati mbaya isipokuwa ni mambo yaliyopangwa na Chadema katika mkakati wa
kutimiza moja ya malengo yao.
Alisema ilikua ni lazima watafute mahali pa
kufanya kituko bungeni ili iwe mjadala na ili wapate sababu na picha za
kuonyesha kwa waliowapa pesa kuwa wanapambana.
"hili
walilofanya Chadema bungeni ni jambo walilopanga katika mkakati wao wa 'civil
disobidiency' ...machafuko ya umma dhidi ya dola, mkakati ambao unaratibiwa
kutoka nje na baadhi ya wale waliokuwa wakoloni katika nchi zetu za Afrika.
Lengo ni kusababisha machafuko na nchi kutotawalika" alisema Nape.
Nape alisema
ndio maana CCM ilisisitiza lazima bunge liendelee kuonyeshwa na televisheni ili
kuonyesha yanayoendelea bungeni kuwawezesha wananchi kuona kinachofanywa na
wawakilishi wao.
"bila
shaka wananchi mmeona kilichotokea bungeni kwa macho yenu, sina haja ya
kuwaeleza. Mmeona wabunge wa upinzani walichofanya,uchaguzi ujao tupunguze
idadi ya vichaa bungeni ili kodi zetu zitumike vizuri,kwani tuliwatuma
wakajadili maendeleo yetu wao wamegeuza bunge uwanja wa masumbwi.
![]() |
| Katibu wa NEC ya CCM itikadi na Uenez. |
"Hoja
iliyowafanya wapigane bungeni haina mashiko, wanataka idadi iongezwe ya wabunge
wa bunge la katiba kutoka 357 mpaka 792. Hivi nani anabeba mzigo huu wa
kuwalipa hawa wabunge kama sio mwananchi wa kawaida? Halafu mnajiita watetezi
wa wanyonge? Hamuoni aibu?" alihoji Nape.
Akiendelea
kufafanua Nape anasema,"
katika hali ya kawaida tungetegemea wajenge hoja ya kundi kubwa katika jamii ya
kitanzania ambao ni wakulima na wafanyakazi ndio wawe na uwakilishi mkubwa
kwenye hilo bunge kama tunataka katiba kweli ya wananchi lakini badala yake wao
wanapendekeza wawakilishi kutoka vyama vya siasa ukiacha wabunge waliopo sasa
wawe 72 na wakulima wawe 10 tu! Wanataka katiba ya vyama vya siasa badala ya
katiba ya nchi kwa ajili ya wananchi. Wanataka wafugaji wawe 10 tu na
wafanyakazi 40. Kwa uwiano wa kawaida asilimia 80% wa wananchi wa nchi hii ni
wakulima, tungetegemea wangependekeza idadi yao kuwa kubwa lakini wao
wanawapuuza wakulima na wafugaji kwa kudai wawe kumi tu"!
Nape
alimalizia kwa kudai kuwa siku za vyama kama Chadema zinahesabika maana hii ya
katiba ndio ilikuwa karata yao ya mwisho.
"
Nimalizie kwa kuwatahadharisha vijivyama hivi vingine kama CUF, NCCR mageuzi na
wengine kuwa wenzao wamepewa mapesa wao wanwaunga mkono kwa ajenda
iliyojificha.
Na kwakuwa hili la kuvuruga katiba ndio karata yao ya mwisho basi
tutarajie anguko baya sana kwa Chadema na huo ndio utakuwa mwisho
wao"!alimalizia Nape.
Source:Mjengwa Blog.
Source:Mjengwa Blog.







No comments:
Post a Comment