![]() |
Anthonia Ojo (25)
akitoa madawa ya kulevya katika makopo ya poda na shampoo baada ya kukamatwa akijianda
kusafiri nazo hadi Rome Italia kupitia ufaransa.
|
![]() |
Mzigo
aliodakwa nao Anthonia Ojo huu hapa.…na Hata hivyo kete hizo 99 hazikujulikana
ni za aina gani.
|
![]() |
Anthonia Ojo
(25) akitoa madawa ya kulevya katika makopo ya poda na shampoo baada ya
kukamatwa.
|
![]() |
Madawa
aliyonaswa nayo Ojo baada ya kutolewa kwenye makopo na yatapelekwa kwa ofisi ya Mkemia
Mkuu wa Serikali ili kubaini aina ya dawa hizo, thamani yake na hatimaye
atafikishwa mahakamani.
|
![]() |
Madawa
aliyonaswa nayo Ojo baada ya kutolewa kwenye makopo.
Credit:
Robert Okanda
|
Mwanamke
mmoja Anthonia Ojo (25), raia wa Nigeria akiwa na kete 99 za madawa ya kulevya
amekamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es
Salaam jana(Septemba 04,2013), akieleke Roma, Italia kupitia Paris, Ufaransa kwa ndege ya
Ethiopian Airways.
Mwanamke
huyo aliingia hapa nchini Agosti 30 akitokea nchini Nigeria na baada ya
kuhojiwa alidai kuwa dawa hizo alizinunua maeneo ya Magomeni, jijini Dar es
Salaam.
Kwa
mujibu wa Kaimu Kamanda wa Viwanja vya Ndege, Renatus Chalya, Ojo anaendelea
kubaki chini ya ulinzi wa polisi kwa uchunguzi zaidi, wakati madawa hayo
yakipelekwa kwa ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini aina ya dawa hizo,
thamani yake na hatimaye atafikishwa mahakamani.
Kete
hizo 99 za dawa za kulevya alikuwa amezihifadhi kwenye chupa ya mafuta ya
kupaka na nyingine kwenye kopo la poda za watoto.
Amesema
kukakamtwa kwa dawa hizo kunafuatia uwanja huo kufungwa mashine za kisasa za
kukagulia mizigo ikiwemo dawa za kulevya.
Aidha
pia raia mmoja wa Urusi aitwae Romani
Demichenco akitokea Berlin Ujerumani kupitia Doha - Qatar amekamatwa kwenye
uwanja wa ndege Dar es salaam akiwa na vivimiminika vinavyoweza kusababisha
milipuko ambapo tayari amefikishwa Mahakamani.
Kukamatwa
kwa Watuhumiwa hao, kumekuja wiki tatu tangu Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison
Mwakyembe, kutangaza vita dhidi ya watu wanaopitisha dawa za kulevya katika
idara na taasisi zilizoko chini ya wizara yake.














No comments:
Post a Comment