Magari
hayo yamekaa kwa muda wa siku nne tangu Septemba Mosi,Mwaka huu baada ya nchi
ya Rwanda kuongeza kiwango cha ushuru kutoka Dola za Marekani 152 (Sh240,000) kuwa
Dola 500 (Sh790,000) .
|
Ni Taswira ya msongamano wa malori kwenye kituo cha Forodha cha Rusumo wilayani Ngara mkoani Kagera huku Serikali ya Rwanda ikishusha ushuru kwa wiki
moja.
|
Kitendo
cha nchi ya Rwanda kupandisha ushuru wa magari yatokayo Tanzania kuingia nchini
humo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) baadhi ya madereva wa kitanzani
watokao bandari ya Dar es Salaam kusafishisha mizigo kwenda katika mchi hizo
wamekwama kwa siku nne kwenye kituo cha forodha cha Rusumo wilaya ya Ngara
mkoani Kagera.
Mmoja
wa madereva hao Ally Rashid Masoud anayefanya
Kazi katika kampuni ya Halgan Transport ya Jijini Dares Salaam amesema kuwa tangu
Septemba Mosi,Mwaka huu wamekaa mpakani hapo na mizigo ndani ya magari bila kupata ufumbuzi wa tatizo hilo.
Masoudi
amesema kuwa wanaoendesha magari ya mizigo kutoka bandari ya Dar es Salamu kuelekea
katika nchi za Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kupitia mpaka wa Rusumo wamekwama kwa siku nne
katika kituo cha Forodha cha Rusumo
wilayani Ngara mkoani Kagera baada ya kupandishiwa ushuru wa magari kuingia
nchini Rwanda.
Kwa
upande wake Afisa Mfawidhi wa kituo cha Forodha cha Rusumo wilayani Ngara mkoani Kagera bw.Nassoro
Ibrahim amesema tangu tozo hiyo ianze msululu wa magari kukaa katika kituo
hicho umekuwa mkubwa ukilinganisha na
awali kabla ya ongezeko la ushuru huo.
Bw.Nassoro
Ibrahim anasema kuwa Septemba Mosi,Mwaka huu,Magari katika kituo hicho yalikuwa
63 ambapo Hadi Jana(Septemba 3,2013) Magari yalifikia 194 na kufanya
Jumla kwa siku tatu Kufikia magari 332.
Hata
hivyo amesema kuwa kwa sasa serikali mbili kati ya Tanzania na Rwanda wako
kwenye mazungumzo ya kusitisha zoezi hilo la kupanda kwa ushuru ili kujenga
mahusiano na kukuza uchumi wa kibiashara bila kuleta madhara kwenye jamii za
nchi hizo.
Wakati
huo huo, Balozi wa Rwanda nchini Tanzania ,Bw.Ben Rugangazi alisema kuongezwa
kwa ushuru huo wa forodha kisichukuliwe kama jaribio la kutaka kuvuruga
uhusiano kati ya nchi hizi mbili.
Balozi
Rugangazi alisema Rwanda imeamua kupandisha kiwango chake kutoka Dola za
Marekani 152 (Sh240,000) kuwa Dola 500 (Sh790,000) ambazo pia hutozwa na
Serikali ya Tanzania kwa muda mrefu.
Amesema
Kumekuwa na majadiliano ya muda mrefu ili kuleta ulinganifu wa ushuru wa
forodha kwani kwa muda mrefu wafanyabiashara Rwanda wamekuwa wakilalamika
kutokana na kushindwa kushindana vizuri kwenye soko la biashara kutokana na
tofauti kubwa ya ushuru wa forodha.
Balozi
Rugangazi anasema Sasa tumeamua kuchukua hatua hii ili kwenda sambamba na
wenzetu Tanzania na pande zote Tanzania na Rwanda zilikubaliana kuwa ushuru
mpya ungeanza kutumika Septemba mwaka huu.
Aidha
Kutokana na msongamano wa malori kwenye mpaka wa nchi hizo mbili, Serikali ya
Rwanda imeshusha ushuru kwa wiki moja.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini Dodoma jana(Septemba 03,2013), Naibu Waziri wa
Uchukuzi, Dk Charles Tizeba alisema ushuru unaotumika ni ule wa zamani badala
ya mpya.
Tizeba
alisema alishauriana na Waziri wa Miundombinu wa Rwanda, Profesa Silas
Rwakabamba na kukubaliana ushuru wa zamani utumike wakati Serikali hizo
zikiendelea na mashauriano.
Alisema
Mawaziri wa Fedha wa Tanzania na Rwanda walitazamiwa kukutana ili kuzungumzia
suala hilo.
Dk
Tizeba alisema wafanyabiashara wa
Tanzania walipata usumbufu mkubwa baada ya kulazimika kulipa Dola 500 kuingiza
mizigo yao Rwanda badala ya Dola 152.
Hata
hivyo, alikanusha madai kuwa Rwanda imepandisha ada hizo kutokana na mgogoro wa
kisiasa baina ya nchi hizo.
Habari/Picha Na:Mwanawamakonda na Shaaban Ndyamukama.
No comments:
Post a Comment