![]() |
Moshi
mkubwa ukitoka katika meli hiyo baada ya wahusika kujitosa majini.
|
![]() |
MV
Gold Star ikipelekwa katika Bandari ya Sicilia.
|
MELI
iliyosajiliwa nchini Tanzania ya MV Gold Star juzi(Septemba 06,2013), Ijumaa
imekamatwa nchini Italia ikiwa na dawa za kulevya zenye thamani ya pauni
milioni 50 sawa na shilingi bilioni 126. 5.
Watuhumiwa
waliokuwa ndani ya meli hiyo waliamua kuichoma moto ili kupoteza ushahidi na
kuamua kupiga mbizi majini lakini walitiwa nguvuni na wanausalama wa Italia.
Meli
hiyo ya mizigo ilikuwa imepakia tani 30 za madawa na ilikamatwa jirani na
Kisiwa cha Sicilia katika Bahari ya Mediterranian nchini Italia wakati
ikielekea Uturuki.
Maofisa
wa polisi nchini humo wamedai kuwa watuhumiwa tisa waliokamatwa ni raia wa
Misri na Syria na watafikishwa mbele ya sheria.
Moto
katika meli hiyo umezimwa na tayari imepelekwa katika Bandari ya Sicilia.
![]() |
| Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda. |
Katika
Hatua Nyingine, Waziri Mkuu wa Tanzania ,Bw. Mizengo Pinda amesema kumekuwa na
changamoto ya uharakishaji wa mashauri ya dawa za kulevya hali inayoifanya
Serikali kufikia hatua ya kufikiria kuwa na mahakama maalumu.
Pinda
aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma, wakati akiahirisha Mkutano wa 12 wa Bunge
hadi Oktoba 29 mwaka huu.
“Nina
imani tukijipanga vizuri inawezekana. Iko hoja kwamba, labda tutafika mahala
tufikirie kuwepo na mahakama maalumu ya dawa za kulevya ambayo itakuwa na kazi
moja tu ya kusimamia mashauri yanayohusu dawa za kulevya,” alisema.
Alisema
pia vita vya dawa za kulevya ni shirikishi kwa kwa mataifa mbalimbali duniani
na kwamba jitihada hizo hufanywa kwa mikutano ya pamoja.
Pinda
alisema hii itasaidia misako ya pamoja, mafunzo ya pamoja na matumizi ya vifaa
mbalimbali kupangwa.
Vilevile,
alisema jitihada nyingine ni kuhamasisha kutunga sheria kali zinazofanana ili
kutotoa mwanya kwa watuhumiwa kupenya na kufikisha dawa za kulevya kwa
watumiaji.
“Ni
kweli kwamba, vita vya dawa za kulevya haviwezi kukomeshwa na nchi moja, kwa
hiyo mapambano dhidi ya wafanyabiashara haramu wa dawa za kulevya yatafanikiwa
tu, kwa nchi zote duniani kuungana kudhibiti biashara hii,” alisema.
Aliwataka
wananchi wote kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, kuwafichua na kutoa
taarifa za wote wanaojihusisha na biashara hiyo.
Waziri Pinda
alisema kati ya mwaka 2010 hadi Julai, 2013, mashauri 368 yanayohusu dawa za
kulevya yalipelekwa mahakamani, kati ya hayo, 91 yalimalizika kwa watuhumiwa
kufungwa na wengine kutozwa faini.
“Kwa
sasa kuna takriban mashauri 245 ambayo bado yako mahakamani. Changamoto
inayotukabili katika mahakama zetu na Jeshi la Polisi ni kuharakisha mashauri
hayo,” alisema.
Pinda
alitumia muda huo pia kueleza kwamba anaiombea Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
ijazwe hekima na Mwenyezi Mungu, akisema kazi ya utungaji sheria ni ya wabunge
wote.
Alisema
hayo kutokana na kitendo cha wabunge hao wa upinzani kususia upitishwaji wa muswada
wa Katiba Mpya.










No comments:
Post a Comment