LIGI KUU VODACOM: Simba yatafuna miwa ya Mtibwa huku Yanga SC na Azam FC hoi…..’’ - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, September 15, 2013

LIGI KUU VODACOM: Simba yatafuna miwa ya Mtibwa huku Yanga SC na Azam FC hoi…..’’

Mashabiki wa Simba SC kwa raha zao Taifa leo, Dar es Salaam na kuichapa Mtibwa Sugar Bao 2-0. 

Kikosi cha Simba SC kilichoanza leo dhidi ya Mtibwa Sukari.

Kikosi cha Mtibwa Sukari  kilichoanza leo dhidi ya Simba SC.

Mashabiki wa Mbya City wakishangilia mchezo wa timu yao na Mabingwa Watetezi Yanga Uwanja wa Sokoine Mbeya na kutoka Sare ya Bao 1-1 na Timu ngumu ya Mbeya City

Kikosi cha Mbeya City kilichoanza leo dhidi ya Yanga SC.

Kikosi cha Yanga SC kilichoanza leo dhidi ya Mbeya City 
 Ligi kuu soka nchini Tanzania (LIGI KUU VODACOM)Leo (Septemba 14,2013) ilikuwa dimbani na Mabingwa Watetezi Yanga walikuwa huko Uwanja wa Sokoine Mbeya na kutoka Sare ya Bao 1-1 na Timu ngumu ya Mbeya City, wenzao Simba walikuwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuichapa Mtibwa Sugar Bao 2-0 na huko Kaitaba Mjini Bukoba Kagera Sugar ilitoka Sare Bao 1-1 na Azam FC.

Huko Mbeya, Wenyeji Mbeya City walitangulia kupata Bao katika Dakika ya 49 alilofunga Bwigane Yeya na Didier Kavumbagu kuisawazishia Yanga katika Dakika ya 71.

Azam Fc nao waliponea chupuchupu baada ya kutanguliwa na Kagera Sugar kwa Bao la Themi Felix katika Dakika ya 25 na Khamis Mcha kurudisha katika Dakika ya 55.

Kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Simba waliipigiga Mtibwa Sugar kwa Bao za Henry Joseph Dakika ya 67 na Betram Mombeki Dakika ya 89.

Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Themi Felix Buhaja alitangulia kuifungia Kagera Sugar dakika ya 25 kabla ya Khamis Mcha ‘Vialli’ kuisawazishia Azam FC dakika ya 55.

Katika mechi nyingine Coastal Union ilitoka sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Ruvu Shooting iliifunga 1-0 Mgambo Shooting bao pekee la Elias Maguri dakika ya 53 Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani, Oljoro JKT ilitoka sare ya 1-1 Rhino Rangers Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, wenyeji wakilazimika kusawazisha dakika ya 27 kupitia kwa Amiri Hamad baada ya Saad Kipanga kutangulia kuwafungia wageni dakika ya tano, wakati Ashanti United ililala 1-0 mbele ya JKT Ruvu, Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam bao pekee la Amos Mgisa dakika ya 81.

Matokeo hayo, yanamaanisha JKT Ruvu inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi zake tisa baada ya kushinda mechi zote tatu, ikifuatiwa na Simba SC katika nafasi ya pili yenye pointi saba.

Timu nyingi zimefungana kwa pointi tano katika nafasi ya tatu, zikiwemo Yanga, Azam na Coastal Union.

RATIBA LIGI KUU VODACOM 2013/2014.
Septemba 18

Tanzania Prisons v Yanga

Simba v Mgambo JKT

Kagera Sugar v JKT Oljoro

Azam FC v Ashanti United

Coastal Union v Rhino Rangers

Mtibwa Sugar v Mbeya City


Ruvu Shootings v JKT Ruvu

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad