Si jambo geni katika karne hii ya sayansi na teknolojia kusikia utapeli
unaofanywa kwa njia ya internet.Ila ni jambo la kuhuzunisha kuwa hata mwaka huu wa 2013 bado watu wanaotapeliwa kirahisi sana kwa mbinu za muda mrefu ambazo endapo tutajenga tabia ya kusoma, kujifunza na kuzingatia, hatutatapeliwa kirahisi. Mbinu zinazohusisha kudanganywa kuhusu urafiki na hata ahadi za ndoa kwa mtu mliyefahamiana kupitia mitandao ya kutafuta marafiki ambao watakuwa wapenzi 'dating sites' kwa lengo la kugeuka wachumba kadiri watakavyoivana na hatimaye kufunga ndoa ni za muda mrefu sasa. Leo nikitizama kipindi cha Dk Phil nimeshangazwa na ushuhuda wa wanawake watatu waliotapeliwa kiasi kikubwa cha fedha na bado walikuwa na imani kuwa iko siku wataonana na watu hao na siyo utapeli. Mwanamke mmoja ameeleza jinsi alivyowasiliana na mwanaume aliyejitambulisha kuwa ni mwanajeshi wa Jeshi la Marekani aliyeko vitani nchini Afghanistan. Akasema mwanaume huyo alijitambulisha kwa ubin wa jina la Advisor, mzaliwa wa Houston, Texas. Timu ya Dk Phil ikachukua vitabu vyote vya posta ili kutafuta jina la "Advisor" na ajabu ni kuwa halikupatikana hata jina moja, si tu katika kitabu cha orodha ya majina cha Texas, bali pia katika vitabu vya majimbo 50. Dk Phil alikuwa akijaribu kumwelewesha mama huyo kuwa hiyo pekee ni dalili ya kuwa mtu huyo hayupo (does not exist). Timu ya Dk Phil ilikwenda mbali kwa kujaribu kutafuta kwenye mitandao mbalimbali majina ya mtu anayejiita 'Advisor' na ilifanikiwa kupata majina zaidi ya 26 kwenye tovuti tofauti, yote yakiwa na picha na maelezo ya mtu yule yule mmoja. Hapa nako Dk Phil alijaribu kumwelewesha mama huyo kuhusu matapeli kutumia majina tofauti tofauti ili kukamilisha lengo lao. Mwishowe Dk Phil alichambua ujumbe kwenye 'chat session' kati ya mama huyo na 'Advisor' ambapo alimweleza makosa makubwa ya kiuandishi ambayo mzaliwa wa Marekani na Texas hawezi kuyafanya, na jinsi ambavyo aina hiyo ya uandishi inatumiwa na matapeli kutoka nchi za Asia au Magharibi mwa Afrika.
Alimwelewesha pia kuwa lengo la tapeli huyo kukataa kuzungumza kwenye
simu siyo kama alivyosingizia kuwa katika eneo la mapigano alipo hairuhusiwi
kuwasiliana na raia hivyo anajiiba kwa kutumia chat, bali ilikuwa ni mbinu ya
kuzuia asigundulike kirahisi lafudhi yake ambayo ingetilia mashaka uraia wake
wa Texas.
Tapeli huyo baadaye alimhadaa kuwa anaweza kuzungumza ila amezuiliwa mahali kutokana na matatizo na hivyo anasubiri kuokolewa. Dk Phil aliamua kupiga namba ya simu ambayo tepeli huyo alikuwa anaitumia kumpigia huyu mama, na hapo Dk Phil akamwuliza yeye ni raia wa Texas katika eneo lipi la Houston? (tapeli akakata simu), Dk Phil akampigia tena, akamwambia mawasiliano huenda mabovu, ila anapenda kufahamu anwani yake ili amsaidie kutoka alikotekwa nyara, mara hii pia tapeli alikata simu.
Muda wote huu akizungumza, lafudhi
yake ilikuwa si ya Kimarekani wala Kimexiko (nchi inayopakana na Texas) bali
ya watu ambao baadhi yetu tumezoea kuzisikia lafudhi hizo kwenye sinema za
Afrika Magharibi.
Mwanzoni mwa uhusiano wao huo, tapeli 'Advisor' alimwambia mama huyu jina la hospitali alikozaliwa, shule ya awali alikosoma n.k., lakini mara zote Dk Phili alipofuatailia taarifa hizi, si jina la hospitali, wala shule ya awali wachilia mbali chuo vilionekana kwa jina lolote.
Hapa nako Dk Phil akatumia
njia hii kumwelewesha mama huyu kuwa huu ni utapeli. Haiwezekani mtu azaliwe
katika hospitali ambayo hakuna aliyewahi kuisikia, ama asome katika shule
ambazo hazijawahi kuwa kwenye rekodi wala kusikika katika eneo hilo.
Dk Phil alipomwuliza mama huyo kuhusu kumbukumbu za fedha alizomtumia tapeli 'Advisor', aliorodhesha mara na kiasi cha fedha anchokumbuka kutuma kwa tapeli huyo kila alipotohadaa. Jumla yake ilikuwa dola za Kimarekani elfu sitini na tatu na ushee (takriban shilingi 100,000,000/= za Tanzania). Mara zote hizo alizotuma fedha alikuwa anaamini kuwa anamsaidia 'Advisor' ambaye alimwahidi kuwa kuna kontena lenye dhahabu za thamani ya dola za Kimarekeni milioni moja, ambazo zitatumwa kwake na hivyo angeweze kurejesha fedha zake zote alizomtumia.
Kwa bahati mbaya, mama huyu na wengine ambao wametapeliwa (na pengine
watakaotapeliwa siku zijazo), ni miongoni mwa wale wasiofahamu wala kujifunza
kung'amua mbinu za kitapeli zinazotumiwa sana katika kudanganya watu na
kuwaibia.
Tapeli wa mama huyu alitumia njia rahisi ya kuzisoma hisia zake na
kujua angekuwa mwepesi wa kuanguka mtegoni wa maana alikuwa anatafuta penzi
(desperate for love) hivyo alimtumia maneno ya mapenzi aliyoyanukuu kutoka
kwenye mitandao.
Kwa mfano, Dk Phil alichukua baadhi ya maneno aliyoyabandika
'Advisor' kwenye chat session na mama huyo ya tarehe 4 Machi 2013,
kuyakuta neno kwa neno, kituo kwa kituo, kwenye tovuti ya Pigbusters.net
(sasa imehamia youreittoday.com)
Tapeli huyu alitumia picha za mtu halisi ambaye ni mwanajeshi halisi aliyefariki tangu mwaka 1994. Kwa bahati mbaya, hawa matapeli wanaweza kutumia hata tukio baya la kweli na wakaunganisha link ya habari kwenye tovuti marufu kama BBC, CNN n.k., ili uongo wao ufanane na ukweli. Kuna usemi kuwa ukiwa unataka sana kukipata kitu, ni rahisi sana kupoteza fikira, ukaongozwa na hisia na moyo badala ya akili (following your heart and not your mind and reasoning) ni rahisi sana kukubali lolote unaloambiwa ikiwa linakidhi kiu yako. Kisa cha mama huyu na wenziye kinazidi kutukumbusha kuwa:-
1. Kuwa
mjanja, usiwe mwepesi kumwamini kila mtu.
2. Si kila
kiandikwacho mtandaoni kinachosema ni cha kweli basi ni kweli na
uhakika.
3. Mtu
yeyote anayewasiliana nawe na kuanza kuomba kutumiwa fedha, huenda ni tapeli.
4. Dalili za
kutambua utapeli ni pamoja na mtu kuomba umtumie majina yako rasmi, anwani,
tarehe ya kuzaliwa, namba za simu, maelezo ya akaunti za benki na hata
password za email au benki.
5. Unapotumiwa
kiambatanisho kwenye email au chat session, usiwe mwepesi kukifungua kwani
hata firewall na anti-virus zinaweza zisiwe na mbinu ya kung'amua ikiwa kuna
virusi vimefungashwa kwenye kiambatanisho hicho ambacho ukikifungua utakuwa
umefungulia njia virusi kuiba taarifa zako binafsi kama vile kunakili kila
unapo-type password ya kufungua tovuti ya benki ama tovuti zenye taarifa zako
za siri.
Kwa bahati mbaya sana, utapeli huu pia umeziingilia simu za kisasa
(smart phones) na virusi hutumwa kwa njia ya iyo hiyo ama kupitia apps au kwa
kupokea link ya website na kuifungua bila kujua unatembelea tovuti ya virusi.
Source: http://www.wavuti.com |
Thursday, September 12, 2013
Hatusomi, hatujifunzi? Huyu katapeliwa 100,000,000/- na “mpenzi” wa mtandaoni.
Tags
# DONDOO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
DONDOO
Labels:
DONDOO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.








No comments:
Post a Comment