Shirikisho la Soka Duniani FIFA leo (Septemba 12,2013) Limetoa Listi ya Ubora Duniani na Mabingwa wa Dunia, Hispania, bado wako pale pale
wakishika Nambari Wani huku Tanzania ikipanda Nafasi moja na kushika Nafasi ya
127 lakini kwenye 10 Bora kuna mabadiliko makubwa.
Argentina
imeibwagaUjerumani na kuikamata Nafasi ya Pili, Uruguay imepanda Nafasi 5 na
sasa ipo ya 7 huku Portugal ikiporomoka kutoka Nafasi 4 na kutua Nafasi ya 11.
Katika 10
Bora zipo Nchi za Marekani ya Kusini 4.
Kwa Nchi za
Afrika, Nchi ambayo iko Nafasi ya juu kabisa ni Ivory Coast ambayo iko Nafasi
ya 19 ikiwa imeporomoka Nafasi moja na kufuatiwa na Ghana iliyobaki Nafasi ya
24 kama Mwezi uliopita.
Listi ya
Ubora inayofuata itatolewa hapo Oktoba 17.
LISTI YA
UBORA YA FIFA:-20 BORA.
1 Spain
2 Argentina
3 Germany
4 Italy
5 Colombia
6 Belgium
7 Uruguay
8 Brazil
9 Netherlands
10 Croatia
11 Portugal
12 Greece
13 Marekani -USA
14 Switzerland
15 Russia
16 Chile
17 England
18 Bosnia-Herzegovina
19 Côte d'Ivoire
20 Ecuador






No comments:
Post a Comment