![]() |
Baadhi ya
watu waliofanikiwa kukimbilia usalama wao.
|
![]() |
Watoa huduma
ya kwanza wanamsaidia mtu aliyejeruhiwa baada ya shambulio la bunduki katika
soko la Westgate shopping centre, mjini Nairobi Septembea 21, 2013.
|
![]() |
Watu
wakikimbia kujificha wakati polisi wanawasaka washambuliaji walovamia kwa bunduki
soko la Westgate jijini Nairobi, Septemba 21, 2013.
|
![]() |
Baada ya
masaa tano ya taharuki ndani ya jengo hilo milio ya risasi ilikuwa inasikika
ishara ya makabiliano kati ya polisi na wanamgambo hao.
|
![]() |
Polisi wenye
silaha wanawasaka washambuliaji wenye silaha ndani ya soko la Westgate mjini
Nairobi, Septemba 21, 2013.
|
![]() |
Watu
wakikimbia kujificha wakati polisi wanawasaka washambuliaji walovamia kwa bunduki
soko la Westgate jijini Nairobi, Septemba 21, 2013.
|
![]() |
Watu wakikimbia
huku wakiinua mikono juu kutoka soko la Westgate Mall mjini Nairobi Sept. 21, 2013.
|
![]() |
Polisi
anajaribu kuhakikisha hakuna mshambuliaji katika eneo alofika baada ya
shambulio ndani ya soko la Westgate Nairobi Sept. 20, 2013.
|
![]() |
Polisi na Wanajeshi wenye
silaha wanawasaka washambuliaji wenye silaha ndani ya soko la Westgate mjini
Nairobi, Septemba 21, 2013.
|
Hali ni tete
katika jiji la Nairobi ambapo washambuliaji wenye silaha Jujmamosi mchana
walivamia eneo la kifahari la Westgate Mall nje kidogo ya jiji la Nairobi.
Vyombo vya
habari vya Kenya vinaripoti kuwa washambuliaji hao waliokuwa waloficha nyuso
zao walivamia maduka hayo mwendo wa saa sita mchana kwa saa za Kenya na
kuwateka nyara watu kadha.
Wafanyakazi
wengi wamenaswa katika mtafaruku huo huku ikiripotiwa kuwa zaidi ya watu 30
wameuawa.
Polisi wa
Kenya wamewaambia wananchi wasiende eneo hilo ambapo kikosi maalum cha
kijeshi KDF kimepelekewa kuwasaka na
kukabiliana na washambuliaji hao.
Polisi huko
Nairobi wanasema Westgate Mall sasa imedhibitiwa na kikosi maalum cha kijeshi
na kwamba kinafanya upekuzi mkali.
Kuna ripoti
kuwa mshambualiaji mmoja amekamatwa na msako unaendeela kubaini hasa ni nani
waliotekeleza mashambulizi hayo na kwa lengo gani.
Afisaa mmoja
mkuu wa kundi la kigaidi la Alshabaab, ameifahamisha BBC kuwa kundi hilo ndilo
limehusika na shambulizi dhidi ya duka la kifahari la Westage mjini Nairobi
Kenya.
Kwa mujibu
wa Afisaa huyo mashambulizi hayo yalikuwa ya kulipiza kisasi kwa Kenya kwa
kujihusisha na vita vya Somalia ambako wanajeshi wake wanakabiliana na kundi
hilo.
Wanajeshi wa
Kenya wamekuwa nchini humo tangu mwaka 2011 kama sehemu ya juhudi za muungano
wa Afrika kutaka kurejesha uthabiti nchini Somalia.
Afisaa mkuu
wa mambo ya ndani Kenya amesema idadi ya waliofariki ni kumi na moja lakini
shirika la msalaba mwekundu linasema idadi hiyo imefika watu 30 huku zaidi ya
hamsini wakijeruhiwa.
Taarifa
kutoka Ikulu ya Rais Kenya zinasema kuwa mshukiwa mmoja aliyekamatwa alifariki
kutokana na majeraha yake.
Wanamgambo
wa Al Shabaab kupitia kwa mtandao wao wa Twitter , wanasema kuwa Kenya
haikuchukulia kwa uzito onyo walilotoa kwa taifa hilo kwa hatua ya kuwapeleka
wanajeshi wake nchini humo kupambana dhidi yao.
Kundi hilo
limesema limekuwa likitoa onyo mara kwa mara kwa Kenya kuwa ikiwa haitaondoa
vikosi vyake nchini Somalia, athari zitakuwa mbaya mno.
Kupitia
mtandao wao wa Twitter, Al Shabaab limesema kuwa Kenya ilijidai kutosikia onyo
hizo, na kuendelea kuwaua waisilamu wasio na hatia nchini Somalia.
Taarifa hiyo
ya Twitter ilisema kuwa Shambulio la Westgate ni tone tu katika bahari ya mfano
wa yanayowakumba wasomali nchini Somalia.
Taharuki
ilianza hii leo saa saba mchana wakati watu wanaokisiwa kuwa kumi walipovamia
jengo la kifahari la Westgate la kuwapiga risasi kiholela wakenya waliokuwa
wanaendelea na shughuli zao za kawaida.
Kwa mujibu
wa shirika la msalaba mwekundu , takriban watu 30 walifariki kwa kupigwa risasi
au kutokana na majeraha yao na wengine wengi wenye majeraha ya risasi
kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.
Source Na:-BBC/VOA































Hawa Al Shababu wanacho tafuta hakijulikan
ReplyDelete