![]() |
| CHELSEA:-Ushindi huo wa 2-0 unamaanisha Fulham inatimiza miaka 34 bila kushinda Stamford Bridge, Chelsea ikizinduka baada ya vipigo vya Everton na FC Basle. |
Mabao ya
Oscar na Mikel kipindi cha pili yamemaliza ukame wa ushindi ndani ya mechi nne
na kuendeleza rekodi ya Jose Mourinho kutofungwa nyumbani katika Ligi Kuu ndani
ya mechi 63 na ushndi wa kwanza tangu wafungwe na Aston Villa.
Ushindi huu
umewafanya Chelsea wafikishe Pointi 10 sawa na Liverpool lakini wao wako juu
kwa ubora wa Magoli lakini huenda Msimo huu ukabadilika hapo kesho baada ya
Mechi 4 za Jumapili ambapo Chelsea wanaweza kuporwa uongozi.
![]() |
Jose Mourinho
akishangilia ushindi wake wa kwanza mwezi huu ambapo Pia ushindi huu umepokewa
kwa furaha kwa wadau wa Chelsea baada ya kufungwa mfululizo Mechi mbili
zilizopita.
|
![]() |
Mwenye timu
tabasamu latosha: Roman Abramovich akiwa jukwaani kuangalia ushindi wa timu
yake.
|
![]() |
Oscar
alituliza mchecheto wa Chelsea baada ya Kipa David Stockdale kutema shuti la
Samuel Eto'o na yeye kufunga.
|
![]() |
| LIVERPOOL:- Wachezaji wa Liverpool wakiangalia mpira uliopigwa kwa kichwa na Lovren ukitinga nyavuni. |
BAO pekee la
Dejan Lovren limeipa Southampton ushindi wa 1-0 Uwanja wa Anfield dhidi ya
wenyeji Liverpool Jana(Septemba 21,2013).
Mwanasoka
huyo wa kimataifa wa Croatia alifunga bao hilo dakika ya 54 na kumaliza rekodi
ya Liverpool kutofungwa ndani ya mechi 12.
Pamoja na
hayo The Saints, inabidi wamshukuru refa Neil Swarbrick aliyewanyima Liverpool
penalti baada ya beki wao kumuangusha Daniel Sturridge kwenye eneo la hari kipindi
cha kwanza.
![]() |
Dejan Lovren
amfunga bao pekee la ushindi dhidi ya Liverpool na hapo akishangilia mbele ya
mashabiki wa Southampton.
|
![]() |
Daniel
Sturridge aisikitika baada ya kupoteza nafasi ya kufunga katika mchezo huo
ambao Liverpool wameupoteza kwa kufungwa bao 1-0.
|
![]() |
Mshambuliaji
Luis Suarez, alikuwepo jukwaani akishuhudia mechi yake hiyo ya mwisho katika
adhabu ya kufungiwa mechi 10 na sasa anarejea uwanjani.
|
LIGI KUU
UINGEREZA MATOKEO.
Jumamosi 21
Septemba,2013.
![]() |
Hasira:
Brendan Rodgers.
|
Norwich City
0 Aston Villa 1
Liverpool 0
Southampton 1
Newcastle
United 2 Hull City 3
West
Bromwich Albion 3 Sunderland 0
West Ham
United 2 Everton 3
Chelsea 2
Fulham 0
RATIBA
[Saa za
Bongo]
Jumapili 22
Septemba,2013.
15:30
Arsenal v Stoke City
15:30
Crystal Palace v Swansea City
18:00
Cardiff City v Tottenham Hotspur
18:00
Manchester City v Manchester United
MSIMAMO-TIMU ZA JUU 2013/2014 :- EPL.
NA
|
TIMU
|
P
|
PTS
|
1
|
Chelsea
|
5
|
10
|
2
|
Liverpool
|
5
|
10
|
3
|
Arsenal
|
4
|
9
|
4
|
Tottenham
|
4
|
9
|
5
|
Everton
|
5
|
9
|
6
|
Southampton
|
5
|
8
|
7
|
Man. City
|
4
|
7
|
8
|
Man. United
|
4
|
7
|
9
|
Stoke City
|
4
|
7
|
10
|
Hull City
|
5
|
7
|






















No comments:
Post a Comment