Lori lenye
namba za usajili T97 AJL lenye tela
namba T746 BKF lilipo acha njia na kupinduka leo (Agosti 02,2013) Mchana na kuziba njia
katika Mlima Mbalizi-Mbeya.
|
Lori likishindwa kupita baada ya Mafuta kumwagika
Barabarani na kusababisha barabara kushindwa kupitika.
|
Magari
yakipita kwa shida baada ya Lori kudondoka.
|
Askari
wakijitahidi kukabiliana na watu waliokuwa wanachota mafuta.
|
Shughuli za
uokoaji zikiendelea kulia ni Dereva wa Lori hilo baada ya kunusurika.
|
Dereva wa
gari hilo Hassan Abdi (35) akiwa haamini kilicho tokea baada ya Kunusurika kifo.
|
YALE YALE!!!
Wananchi wenye ndooo Haya.... Wenye
Madumu haya .... wenye Masefuria haya... wote walikuwepo kuchota Mafuta kama
inavyo onekana ... bila kujali kama yaweza kulipuka.
|
Wananchi
Mbalimbali wakiwa wanapata shida kupita baada ya Lori kudondoka.
|
Askari wa
zima moto wakiwa wanaendelea na Juhudi za kuondoa mafuta barabarani kwa maji.
|
Wananchi
mbalimbali wakiwa wanaondoka na Mafuta... huku wengine wakiendelea kuchota.
|
Wakina
mama... Watoto... Vijana na wazee wakiwa wanapata shida jinsi ya kupita baada
ya ajali.
|
Kushoto ni
Tingo Saimoni Msovela (23) na dereva wake Hassan Abdi wakijitahidi kuziba
mafuta yasiendelee kuvuja.
|
Tingo wa
Lori hilo la mafuta baada ya kuokolewa kutoka kwenye Gari.
|
Watu wawili
wamenusurika kifo baada ya roli la mafuta lenye namba za usajili T 978 AJL
lenye tela namba T 746 BKE Aina ya SCANIA walilokuwa wakisafiria kutoka DAR ES
SALAAM kwenda ZAMBIA kuacha njia na kupinduka katika mteremko wa MBALIZI
barabara MBEYA TUNDUMA leo(Agosti 02,2013).
Dereva
ametambuliwa kwa jina la HASSAN ABDI 35 na msaidizi wake SAIMON SOVELA 23 ambao
walikuwa wametokea DAR ES SALAAM kuelekea ZAMBIA likiwa limejaa shehena ya
mafuta.
Kwa mujibu
wa Dereva amesema kuwa gari hilo ghafla lilipoanza kuteremka mteremko
liliharibika mfumo wa breki na mbele yake kukiwa na magari matano baada ya
kuona kuwa angesababisha maafa makubwa aliamua kulichepusha pembeni ndipo
lilipoacha njia na kupinduka na kumwaga shehena ya mafuta.
Kikosi cha
zimamoto kilifika eneo la tukio na kuhakikisha usalama wa eneo hilo kuhofia
mlipuko wa moto ambao ungeweza kutokea kutokana na baadhi ya wananchi kuanza
kuchota mafuta yaliyokuwa yanatiririka.
Pamoja na
juhudi za Jeshi la Polisi kudhibiti wananchi kutochota mafuta lakini wananchi
walikaidi na kuendelea kuchota mafuta.
Ajali hiyo
ilisababisha adha kubwa kwa wasafiri waliokuwa wana pita barabara hiyo wakiwemo
wagonjwa na waliokuwa wanawahi usafiri wa ndege majira ya saa saba mchana.
Na Mbeya
yetu Blog.
No comments:
Post a Comment