Hii ndio Taswira na Matokeo halisi ya Ligi Kuu soka Vodacom,Uingereza,Italia na Ujerumani 2013/2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, August 25, 2013

Hii ndio Taswira na Matokeo halisi ya Ligi Kuu soka Vodacom,Uingereza,Italia na Ujerumani 2013/2014.

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Vodacom, Yanga SC Jana(Agosti 24,2013) wameanza kampeni yao ya kutetea Taji lao huko Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kwa kuitwanga Timu iliyopanda Daraja Msimu huu, Ashanti United, Mabao 5-1.


Bao za Yanga SC zilifungwa na Jerry Tegete, Bao 2, Msuva, Niyonzima na Nizar Khalfan wakati lile la Ashanti lilifungwa na Shaban Juma alieingizwa Kipindi cha Pili.

Wachezaji wa Yanga wakiwa katika Picha ya pamoja na  wameanza kampeni yao ya kutetea Taji lao la Ligi kuu Vodacom huko Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kwa kuitwanga Timu iliyopanda Daraja Msimu huu, Ashanti United, Mabao 5-1.

Kikosi cha Jana(Agosti 24,2013) cha Coastal Union,  hiki kilichoanza dhidi ya Oljoro JKT na waliichapa JKT Oljoro Bao 2-0 kwa Bao za Abdi Banda.

Wachezaji wa Timu za Mbeya City na Kagera Sukar wakisalimia kabla ya kuanza mchezo wao katika Uwanja wa Sokoine ambapo timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.
Huko Manungu, Mtibwa Sugar na Azam FC zilitoka Sare Bao 1-1 huku Mtibwa wakitangulia kufunga katika Dakika ya 4 kwa Bao la Luizio na Azam FC kusawazisha katika Dakika ya 33 kwa Bao la Penati ya Aggrey Morris.

Nao Coastal Union, wakicheza Ugenini huko Arusha, waliichapa JKT Oljoro Bao   2-0 kwa Bao za Abdi Banda, Dakika ya 10, na Bao jingine la Dakika ya 29 ni la kujifunga wenyewe JKT Oljoro.

Toka Tabora, Timu mpya Rhino Rangers ilitoka Sare ya Bao 2-2 na Simba SC huku Bao zote mbili za Simba SC zikifungwa kwa Penati za Jonas Mkude na Bao za Rhino kufungwa na Noel na Kipanga.

LIGI KUU VODACOM 2013/2014.
Jumamosi Agosti 24,2013.

Yanga 5 Ashanti 1
Mtibwa Sugar 1 Azam FC 1
JKT Oljoro 0 Coastal Union 2
Mgambo JKT JKT Ruvu
Mbeya City 0 Kagera Sugar 0
Ruvu Shooting 3 Prisons 0
Rhino Rangers 2 Simba 2

RATIBA YA LIGI KUU VODACOM:
Jumatano Agosti 28,2013.

Mtibwa Sugar v Kagera Sugar
Rhino Rangers v Azam FC
JKT Ruvu v Prisons
Mbeya City v Ruvu Shootings
Mgambo JKT v Ashanti United
JKT Oljoro v Simba
Yanga v Coastal Union

SERIE A -ITALIA 2013/2014.

AC Milan
Ligi kuu ya SERIE A huko Italia ilianza Jana (Agosti 24,2013) kwa Luca Toni, Mkongwe wa Miaka 36, kuipigia Timu yake iliyopanda Daraja Hellas Verona Bao 2 na kuibwaga AC Milan 2-1 na Mchezaji mpya Carlos Tevez kufunga Bao pekee wakati Mabingwa Juventus walipoifunga Sampdoria Bao 1-0 Ugenini.

AC Milan walitangulia kwa Bao la Dakika ya 14 alilofunga Andrea Poli ambae alikuwa akiichezea Klabu yake mpya Mechi ya kwanza tu.

Lakini vichwa viwili vya Mkongwe Luca Toni, Mchezaji wa zamani wa Kimataifa wa Italy, vya Dakika za 29 na 53 viliipa Hellas Verona ushindi wa Bao 2-1 katika Mechi yao ya kwanza ya Msimu mpya wa Ligi na pia ikiwa ni mara yao ya kwanza kucheza Serie A katika Miaka 11.

Ushindi huo ulileta furaha kubwa na hoihoi kwa Mashabiki wa Hellas Verona waliojazana Stadio Bentigodi ambao kwa Miaka mingi waliteseka wakiona Timu yao ikigaagaa Madaraja ya chini ya Ligi yale ya Pili na ya Tatu wakati Mahasimu wao wakubwa wa Mji mmoja, Chievo Verona, wakimeremeta Ligi kubwa ya Serie A.

Juventus striker Carlos Tevez has admitted he had enjoyed the "perfect night" after scoring on his debut in the 1-0 win over Sampdoria in front of his former Manchester City boss Roberto Mancini.
Huko Mjini Genoa, Bao pekee la Mechi kati ya Wenyeji Sampdoria na Mabingwa Juventus lililofungwa na Carlos Tevez katika Mechi yake ya kwanza kabisa ya Serie A liliipa ushindi Juventus wa Bao 1-0.

Bao hilo llifungwa katika Dakika ya 58 kufuatia kazi nzuri ya Arturo Vidal na Paul Pogba kwenye Kiungo.

Katika Dakika ya mwisho, Sampdoria walibaki Mtu 10 wakati Paolo Castellini, alieingizwa toka Benchi, kumchezea rafu mbaya Stephan Lichtsteiner na kupewa Kadi Nyekundu.

Serie A inaendelea tena leo(Agosti 25,2013)  kwa Mechi 7 na kesho Jumatatu Usiku iko Mechi moja.

SERIE A 2013/2014  RATIBA/MATOKEO.
Jumamosi Agosti 24,2013.

Hellas Verona 2 AC Milan 1
Sampdoria 0 Juventus 1

Jumapili Agosti 25,2013.
[Saa za Bongo]

19:00 Inter Milan v Genoa
21:45 SS Lazio v Udinese
21:45 Parma v Chievo Verona
21:45 Torino FC v Sassuolo
21:45 Napoli v Bologna
21:45 Livorno v AS Roma
21:45 Cagliari v Atalanta

Jumatatu Agosti 26,2013.

21:45 Fiorentina v Catania

LIGI KUU ENGLAND 2013/2014.
  
Daniel Sturridge
Liverpool Jana(Agosti 25,2013) wameendeleza ushindi wao wa pili katika Mechi zao mbili za kwanza za Ligi Kuu England kwa Msimu huu mpya wa 2013/14 baada ya Straika wao Daniel Sturridge kufunga Bao pekee Uwanjani Villa Park na kuwatungua Wenyeji Aston Villa Bao 1-0.

Katika Mechi ya kwanza ya Ligi Jumamosi iliyopita, Liverpool waliifunga Fulham Bao 1-0 na Mfungaji alikuwa Daniel Sturridge.

Bao hilo la Sturridge lilifungwa katika Dakika ya 21 na hilo ni Bao lake la 8 katika Mechi 7 za Ligi alizocheza kuanzia Msimu uliopita.

Mara ya mwisho kwa Liverpool kushinda Mechi zao mbili za kwanza za Msimu mpya ni ule Msimu wa 2008/09.

Ligi Kuu England inaendelea Jumapili kwa Mechi mbili kati ya Cardiff City na Manchester City na nyingine n kati ya Tottenham na Swansea City.

LIGI KUU ENGLAND MATOKEO.
Jumamosi 24 Agosti,2013.

Fulham 1 Arsenal 3
Everton 0 West Bromwich Albion 0
Hull City 1 Norwich City 0
Newcastle United 0 West Ham United 0
Southampton 1 Sunderland 1
Stoke City 2 Crystal Palace 1
Aston Villa 0 Liverpool 1

Jumapili 25 Agosti,2013.

18:00 Cardiff City v Manchester City
18:00 Tottenham Hotspur v Swansea City

Jumatatu 26 Agosti,2013.

22:00 Manchester United v Chelsea

BUNDESLIGA UJERUMANI 2013/2014.

MABINGWA wa Ujerumani , Bayern Munich, Jioni ya jana(Agosti 24,2013) wamepata ushindi wao wa tatu mfululizo kwenye Msimu mpya wa Ligi ya Bundesliga walipoifunga 2-0 Nuremberg Uwanjani Allianz Arena na wao kuwa moja ya Timu 4 ambazo zimeshinda Mechi zao zote za Ligi hiyo tangu ianze.

Timu nyingine ambazo zimeshinda Mechi zote 3 ni Borussia Dortmund, Bayer Leverkusen na Mainz.

Katika Mechi yao ya jana , Bayern Munich walikosa Penati katika Kipindi cha Kwanza iliyopigwa na David Alaba na Kipa wa Nuremberg Raphael Schaefer kuokoa lakini Kipindi cha Pili walifunga Bao zao zote mbili.

Bao la kwanza la Bayern lilifungwa na Franck Ribery kwa kichwa cha Dakika ya 69 na kisha Arjen Robben akapachika Bao la pili katika Dakika ya 78.

  Bayern Munich boss Pep Guardiola paid tribute to match-winners Franck Ribery and Arjen Robben after the pair scored in the 2-0 win over Nurnberg on Saturday.
Katika Mechi hii Bayern walishusha Kikosi kikali kilichokamilika hasa kwenye Kiungo ambapo Mawinga walikuwa ni Robben na Ribbery na katikati walikuwa Viungo Wachezeshaji Thiago Alcantara na Mario Gotze.

Jumanne Bayern watacheza Mechi ya Ligi na Freiburg na Ijumaa wataruka kwenda Monaco kucheza Mechi ya UEFA Super Cup dhidi ya Chelsea.

BUNDESLIGA RATIBA/MATOKEO:
Ijumaa Agosti 23,2013.

Borrussia Dortmund 1 Werder Bremen 0

Jumamosi Agosti 24,2013.

Bayern Munich 2 Nurnberg 1
Hannover 2 Schalke 1
Hoffenheim 3 Freiburg 3
Leverkusen 4 Monchengladbach 2
Mainz 2 Wolfsburg 0
Hertha 1 Hamburg 0

Jumapili Agosti 25,2013.

16:30    Eintracht Braunschweig v Eintracht

18:30    Augsburg v Stuttgart

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad