![]() |
Shujaa wa Yanga SC Jerry Tegete. |
Mabao ya Yanga leo(Agosti 24,2013) yalifungwa na Jerry Tegete dakika za 10 na 57, Simon Msuva dakika ya 47, Haruna Niyonzima dakika ya 73 na Nizar Khalfan dakika ya 90, wakati bao pekee la Ashanti lilifungwa na Shaaban Juma dakika ya 89.
Tegete alifunga bao la kwanza baada ya kupokea pasi ya nyota wa mchezo wa leo, Simon Msuva na kumlamba chenga beki Tumba Sued kabla ya kumtungua kipa Ibrahim Abdallah na lingine alifunga kwa krosi ya Msuva tena na kumvuta kipa kutoka langoni kabla ya kufunga.
Msuva alifunga bao bora zaidi katika mchezo huo, baada ya kuwalamba chenga mabeki wawili wa Ashanti, Tumba Sued na Ramadhani Malima kisha kuutumbukiza mpira kimiani kwa kichwa.
Niyonzima alifunga kwa kichwa akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na beki David Luhende na Nizar alifunga kwa krosi ya Frank Domayo wakati Juma aliipatia Ashanti bao la kufutia machozi baada ya kuwatoka mabeki wa Yanga.
Kikosi cha Yanga SC:- kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Athumani Iddi ‘Chuji’/Frank Domayo dk18, Simon Msuva, Salum Telela, Didier Kavumbangu/Hussein Javu dk67, Jerry Tegete na Haruna Niyonzima.
Ashanti United:- Ibrahim Abdallah, Khan Usimba, Emanuel Kichiba, Ramadhani Malima, Tumba Sued, Emanuel Memba, Fakih Hakika, Mussa Nampaka/Laurent Mugia dk61, Hussein Sued, Mussa Kanyaga/Shaaban Juma dk49 na Joseph Mahundi.
Nako huko Katika Ligi kuu Nchini Uingereza - WAKICHEZA
mapema hii leo kwenye Mechi ya Ligi Kuu England huko Craven Cottage, Arsenal waliifunga
Fulham Bao 3-1 katika Mechi ya Dabi ya Jiji la London huku Lukas Podolski
akiifungia Bao 2 katika mchezo huo.
Wakicheza
kwa kasi kubwa kama ile iliyowapa ushindi wa Bao 3-0 huko Uturuki Juzi Jumatano
walipoifunga Fenerbahce katika Mechi ya kwanza ya Raundi ya Mchujo ya UEFA
CHAMPIONZ LIGI, iliwachukua Dakika 14 kwa Arsenal kupiga Bao la kwanza kupitia
Olivier Giroud.
Mechi
inayofuata ya Ligi kwa Arsenal ni ya Nyumbani kwao Emirates hapo Septemba
Mosi,mwaka huu ikiwa ni Dabi ya London ya Kaskazini dhidi ya Mahasimu wao
Tottenham Hotspur.
VIKOSI:
Fulham: Stockdale, Riether, Hughes,
Hangeland, Riise, Duff, Parker, Sidwell, Taarabt, Kasami, Berbatov.
Akiba: Ruiz,
Kacaniklic, Karagounis, Briggs, Boateng, Etheridge, Bent.
Arsenal: Szczesny, Jenkinson, Sagna,
Mertesacker, Gibbs, Rosicky, Ramsey, Walcott, Cazorla, Podolski, Giroud.
Akiba:
Wilshere, Monreal, Fabianski, Sanogo, Frimpong, Gnabry, Zelalem.
Refa:
Howard Webb
RATIBA YA LIGI KUU ENGLAND 2013/2014.
[SAA NI
ZA BONGO]
Jumapili
25 Agosti,2013.
18:00
Cardiff City v Manchester City
18:00
Tottenham Hotspur v Swansea City
Jumatatu
26 Agosti,2013.
22:00
Manchester United v Chelsea
No comments:
Post a Comment