Watu 21 wamejeruhiwa vibaya na wengine 30 wakinusurika kifo katika Ajali ya Basi la SAI BABA eneo la Vigwaza mkoani Pwani. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, July 02, 2013

Watu 21 wamejeruhiwa vibaya na wengine 30 wakinusurika kifo katika Ajali ya Basi la SAI BABA eneo la Vigwaza mkoani Pwani.


Watu 21 wamejeruhiwa vibaya na wengine 30 wakinusurika kifo baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka jijini Dar es salaam kwenda Mjini Songea kupata ajali eneo la Vigwaza mkoani Pwani.



 Mkuu wa kikosi cha askari wa barabarani Chalinze Assistance Inspector Sule amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa mbili asubuhi ya leo July 02,2013  baada ya basi la abiria la kampuni ya Saibaba lenye namba za usajili T 779 BKL kutaka kulipita gari lingine huku likiwa katika mwendo kasi na hatimaye gari lilimshinda dereva huyo na kisha kupinduka.




Aidha ameongeza kuwa majeruhi hao wamekimbizwa katika hosiptali ya tumbi kibaha kwa ajili ya matibabu na kwamba basi hilo lilikuwa na jumla ya abiria 51.










Habari kwa hisani ya www.mchomeblog.com.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad