Rais Obama alilakiwa na rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na maelfu ya watu pamoja na kundi la
wacheza ngoma na sarakasi katika uwanja wa ndege wa Dar es salaam leo Jumatatu(Julai 01,2013). |
Rais Barack
Obama wa Marekani amewasili Tanzania kwenye kituo chake cha mwisho katika ziara
yake ya nchi tatu za Afrika.
Rais Obama alilakiwa na rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na maelfu ya watu pamoja na kundi la
wacheza ngoma na sarakasi katika uwanja wa ndege wa Dar es salaam leo Jumatatu(Julai 01,2013).
Katika ziara
yake ya siku mbili nchini Tanzania Bw.Obama atafanya mazungumzo na Rais
Kikwete, kukutana na viongozi wa
biashara na kuzungumza na mkutano wa wakuu wa biashara nchini humo .
Rais
Barack Obama wa Marekani
akisakata
ngoma na rais Kikwete.
|
Tanzania ni
moja ya nchi 9 ambazo zitakazoshirikishwa katika juhudi mpya aliyotangaza Rais
Obama Jumapili (Juni 30,2013) kusaidia
kuongeza nguvu za umeme barani Afrika hasa kusini mwa jangwa la Sahara.
Alitangaza
mpango wa dola bilioni 7 katika hotuba yake katika chuo kikuu cha Cape Town
huko Afrika Kusini na kusema itaongeza uzalishaji wa umeme maradufu kwenye bara
hilo.
Pamoja na
Tanzania juhudi hiyo itaanzishwa Ethiopia , Kenya , Liberia na Nigeria Uganda
na Zimbabwe .
Jumapili (Juni
30,2013) Rais Obama alitembelea kisiwa cha Robben ambako Rais wa zamani wa
Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela
alifungwa kwa miaka 18 kati ya miaka 27 aliyokuwa kifungoni kwa mapambano yake dhidi ya kupinga ubaguzi
Afrika kusini.
Taswira
mbalimbali zinazoonyesha maandalizi ya mapokezi makubwa ya Rais wa Marekani
Barack Obama atapowasili Ikulu jijini Dar es Salaam mchana huu.
|
No comments:
Post a Comment