Gari ya mbao iliyobuniwa na mkazi wa kijiji cha Nyololo mkaoni
Iringa, Keneth Mwangoka imeokoa shilingi Bilioni moja kwa mwaka kwa kuhamasisha
kuhifadhi mazingira katika msitu wa Sao Hill ulioko mkoani humo.
Akizungumza na MAELEZO katika viwanja vya Maonesho ya 37 ya Sabasaba
jijini Dar es Salaam jana (Julai 05,2013), Afisa Misitu wa Wizara ya Maliasili na Utalii kutoka
Msitu wa Sao Hill mkoani Iringa, Fidelis Mwanalikungu alisema gari hiyo
ilibuniwa kwa kushirikiana na Kikundi cha Sanaa cha Imehe kilichopo katika
kijiji cha Nyololo.
Alisema kikundi hicho kwa kutumia gari hiyo ambayo huvutia watu
kuiangalia, kinaeleimisha vijini 58 vinavyozunguka msitu wa Sao Hill kudhibiti
matumizi ya moto unawashwa na wakulima wakati wa kuandaa mashamba yao kwa ajili
ya kilimo.
Alifafanua kuwa uhamasishaji huo umefanikiwa kupunguza moto kutoka
matukio 143 yaliyokuwa yanasababisha hekta za misitu 500 hadi 1000 kwa mwaka
hadi kufikia matukiio manne tu kwa mwaka yaliyounguza hekta 17 za misitu.
“Ukiweka hizo hekta 500 hadi 1,000 katika thamani ya fedha unakuta tulikuwa
tunapoteza kuanzia Milioni 840 mpaka Bilioni moja kwa mwaka kutokana na kuungua
kwa msitiu huo, sasa hii ni hasara kubwa” alisema Mwanalikungu.
Alisema kutokana na elimu inayotolewa kushirikisha kikundi hicho,
wameweza kuhifadhi zingira ya msitu huo wa asili wa Serikali, vyanzo vya maji
na kuhifadhi mazingira ya vijiji hivyo.
Aliongeza kuwa kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2009 uliobaini
kuwa kutoka mwaka 2010 kurudi nyuma miaka 11 kulikuwa kuna matukio mengi ya
moto yenye wastani wa matukio 143 kwa mwaka.
“Ilipofika mwaka 2011 tukaangalia ni mikakati gani tunaweza kuichukua kwa
kuwashirikisha wanavijiji, ndipo tukagundua wazo la kusema tukiwa na gari kama
hili linalovutia watu, tukaweka mabango ya kuelimisha tunaweza kufikisha ujumbe
kwa urahisi zaidi” alisema Mwanalikungu.
Akizungumzia gari hiyo, Keneth Mwangoka amesema gari hiyo aina ya
Toyota Hiace aliinunua kutoka kwa mtu ambaye alitaka kuiuza kama chuma
chakavu na aliitengeneza ili iweze kusaidia katika kuwavutia wanajiji na kupata
njia ya kuwapata kwa urahisia wanakijiji a kufikisha ujumbe.
Mwangoka ambaye ni fundi wa gari hiyo, alisema gari hiyo ina injini
ya Toyota 1S, robu tatu ya vitu vilivyotengeneza ni mbao na inatumia mafuta
lita moja kwa kilomita nane.
Nilivutiwa sana na hilo gari la mbao nilipotembelea banda la Maliasili na Utalii! Hivi ndivyo ilivyokuwa...
ReplyDeletehttp://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/07/umewahi-ona-gari-la-mbao.html