Picha za kubomoa Majengo Baada Waziri wa Ujenzi, Pombe Magufuli kutoa maagizo kwenye majengo yaliyo pembezoni mwa barabara ya Ali Hassan Mwinyi ili kupisha upanuzi wa barabara hiyo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, July 07, 2013

Picha za kubomoa Majengo Baada Waziri wa Ujenzi, Pombe Magufuli kutoa maagizo kwenye majengo yaliyo pembezoni mwa barabara ya Ali Hassan Mwinyi ili kupisha upanuzi wa barabara hiyo.


 Baada Waziri wa Ujenzi, Pombe Magufuli kutoa maagizo kwa wenye majengo yaliyo pembezoni mwa barabara ya Ali Hassan Mwinyi, kubomoa wenyewe majengo yao ili kupisha upanuzi wa barabara hiyo, kuonekana yakisua sua, hatimaye (Julai 04,2013) ameanza rasmi kazi ya kubomoa kwa Greda katika majengo ya wale walioonekana kukaidi agizo hilo.



 Katika kutekeleza agizo hilo zoezi hilo limeanzia kwenye Jengo la Business Park (Green Acres) lililopo eneo la Victoria.




 Tayari ukuta ukiwa umeshashushwa chini wa upande wa barabarani  huku baadhi ya watu waliokuwa na  shughuli zao katika jengo hilo wakihaha kuhamisha baadhi ya vifaa.





Watu wakishangaa kama kawaida ya Wabongo  na Huu unaonekana ni upande wa pili wa jengo hilo.


Jamaa wakisimamia usalama pande hizo wakiwafukuza raia waliokuwa wamekusanyika eneo hilo na kuongoza magari kuondoa foleni eneo hilo.



   Katapila likiendelea na kazi ya kubomoa hapa ni jengo la pili lililokaribu na Green Acres nalo likiliwa hapa tayari ukuta ukiwa unashuahwa.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad