Taifa Stars imeshindwa kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani baada ya leo (Julai 13,2013 ) kufungwa bao na Uganda (The Cranes) kuwania tiketi ya kucheza Fainali za (CHAN) mwakani Afrika Kusini. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, July 13, 2013

Taifa Stars imeshindwa kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani baada ya leo (Julai 13,2013 ) kufungwa bao na Uganda (The Cranes) kuwania tiketi ya kucheza Fainali za (CHAN) mwakani Afrika Kusini.



Taifa Stars 0 - 1 Uganda.
Timu ya Soka ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ikicheza Nyumbani Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam  leo(Julai 13,2013) imefungwa Bao 1-0 na  Timu ya Soka ya Taifa ya Uganda  katika Mechi ya kwanza ya kusaka nafasi ya kucheza Fainali za CHAN, African Nations Championship 2014, zitakazochezwa huko Afrika Kusini Januari Mwakani.




Bao la Uganda lilifungwa Kipindi cha Pili Dakika ya 46 na Iguma Dennis.



Mechi ya Marudiano itachezwa huko Uganda baada ya Wiki mbili na Mshindi atakwenda Fainali huko Afrika Kusini. 



VIKOSI:



Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Starz).
TAIFA STARS: Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Kelvin Yondani, Frank Domayo, Mwinyi Kazimoto, Salum Aboubakari, John Bocco, Mrisho Ngassa, Amri Kiemba.





Timu ya Taifa ya Uganda.
UGANDA: Muwonge Hamza, Waswa Hassan, Wadada Nico, Majegwa Brian, Kabugo Savio, Kasaga Richard, Iguma Dennis, Said Kyeyune, Mpande Joseph, Edema Patrick, Odur Tonny



Refa: Thierry Nkurunziza


         

RATIBA  CHAN 2014.



KANDA KASKAZINI  (Timu 2 zitafuzu)



05-07/07/13: Tunisia v Morocco


26-27/07/13: Morocco v Tunisia


Algeria v Libya - Imefutwa


Libya watacheza Fainali huko South Africa baada Algeria kujitoa.




KANDA MAGHARIBI  A (Timu 2 zitafuzu)

Raundi ya Awali 



30/11/12-2/12/12 : Liberia 0-1 Mauritania; Guinea 0-0 Sierra Leone


14-16/12/12: Mauritania 2-1 Liberia; Sierra Leone 1-1 Guinea


Mauritania wamepita Jumala ya Bao 3-1


Guinea wamepita kwa Magoli ya Ugenini 



Raundi ya 1



05-07/07/13: Senegal v Mauritania; Mali v Guinea


26-27/07/13 : Mauritania v Senegal; Guinea v Mali





KANDA MAGHARIBI B(Timu 3 zitafuzu)

Raundi ya Awali


30/11-2/12/12/12: Burkina Faso 2-1 Togo


14-16/12/12: Togo 0-1 Burkina Faso


Burkina Faso wamepita Jumla ya Bao 3-1 



Raundi ya 1


05-07/07/13: Benin v Ghana; Nigeria v Ivory Coast; Burkina Faso v Niger


26-27/07/13: Ghana v Benin; Ivory Coast v Nigeria; Niger v Burkina Faso




KANDA KATI (Timu 3 zitafuzu)

Raundi ya Awali


Central African Republic v Congo - cancelled


Congo inasonga baada ya kujitoa Central African Republic


Raundi ya 1


05-07/07/13: Cameroon v Gabon; DR Congo v Congo


26-27/07/13: Gabon v Cameroon; Congo v DR Congo


Washindi watatinga Fainali



Mchujo Raundi ya 1


Watakaofungwa Mechi za Raundi ya 1 watapambana kati ya Tarehe 26-28/07/13 na 
09-11/08/13 na Washindi wawili kusonga Fainali.
 



KANDA KATI MASHARIKI(Timu 3 zitafuzu)

Raundi ya Awali



14-16/12/12: Burundi 1-0 Kenya; Eritrea v Ethiopia ( Ethiopia wamesonga baada Eritrea kujitoa)


06/01/13: Kenya 0-0 Burundi (Burundi wamesonga Jumla ya Bao 1-0)



Raundi ya 1


05-07/07/13: Burundi v Sudan


12-13/07/13: Ethiopia v Rwanda; Tanzania 0 Uganda 1


26-27/07/13: Sudan v Burundi, Rwanda v Ethiopia, Uganda v Tanzania





KANDA KUSINI (Timu 3 zitafuzu pamoja na Wenyeji South Africa)

Raundi ya Awali



30/11-2/12/12 : Mauritius 2-0 Comoros


14-16/12/12: Comoros 0-0 Mauritius


Mauritius yasonga Jumla ya Bao 2-0



Raundi ya 1


23/06/2013: Swaziland 0-1 Angola


29/06/2013: Angola 1-0 Swaziland


Angola yasonga Jumla ya Bao 2-0


26-7/07/13: Mauritius v Zimbabwe; Mozambique v Namibia; Botswana v Zambia


02-04/08/13: Zimbabwe v Mauritius, Namibia v Mozambique; Zambia v Botswana



Raundi ya 2


26-28/07/13 : Mechi za Kwanza


09-11/08/13: Mechi za Pili


Raundi ya 2


Washindi wawili wa Raundi ya 2 wanaungana na Wenyeji South Africa kucheza Fainali.


Mshindi Mauritius/Zimbabwe v Mshindi Mozambique/Namibia  


Botswana/Zambia v Angola


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad