Nae Neymar alitwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Kombe la Mabara na kuzawadiwa Kiatu cha Dhahabu cha Adidas. |
Mchezaji David
Luiz akiwa na Kombe baada ya sherehe katika uwanja wa Maracana na Kombe la Mabara baada ya kuwafunga mabingwa wa
dunia, Hispania .
|
Alvaro
Arbeloa angepewa kadi nyekundu kwa rafu aliyomchezea Neymar - wachezaji hao
walikuwa peke yao wakati beki huyo wa
Real Madrid alipomuangusha mwenzake.
|
David Luiz
aliokoa kwenye mstari wa goli shuti la Pedro, ambalo kama lingeingia ingekuwa bao
2-1.
|
Hispania
kupitia mchezaji wake Sergio Ramos
alikosa Penati Kipindi cha Pili .
|
Gerard Pique
akionyeshwa kadi nyekundu na Mwamuzi wa Mchezo huo wa fainali kati ya Brazil na
Hispania jana(Juni 30,2013) baada ya
kumuumiza Neymar aliyelala chini.
|
Mwimbaji wa
Colombia, Shakira alikuwepo Rio kumuangalia mpenzi wake, Gerard Pique
akiichezea Hispania.
|
Wenyeji katika Fainali ya Kombe la Mabara ,Timu ya
taifa ya Brazil jana(Juni 30,2013) wametawazwa kuwa mabingwa wa Kombe hilo
baada ya kuwafunga Mabingwa wa Dunia, Hispania kwa mabao 3-0 katika mchezo wa
Fainali ya kombe hilo iliyochezwa uwanja wa Estadio Do Maracana JijinI Rio De
Janeiro Nchini Brazil.
Huku
wakishangiliwa mno na Mashabiki wao Brazil, Mabingwa wa Dunia mara 5,Brazil
walipata bao lao la kwanza katika dakika ya 2 mfungaji akiwa Fred na dakika 47
huku Supastaa Neymar na kumaliza Rekodi ya Hispania ya kutofungwa katika Mechi 29 ya Mashindano
rasmi,akafunga bao la pili kwa shuti kali dakika ya 44 ya mchezo huo.
Hispania
kupitia mchezaji wake Sergio Ramos
alikosa Penati Kipindi cha Pili na Gerard Pique kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu
kwa kumuangusha Neymar yeye akiwa Mtu wa mwisho zikiwa zimesalia Dakika 22.
Mara baada
ya Filimbi ya mwisho kulia, Mashabiki wa Brazil waliimba ‘MABINGWA WAMERUDI!’
huku Mitaa ya Rio De Janeiro ikifurika na Mashabiki waliokuwa wakicheza densi kwa
furaha badala ya kuandamana kwa kahara kama walivyofanya kabla ya Mechi.
Nae Neymar
alitwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Kombe la Mabara na kuzawadiwa Kiatu cha
Dhahabu cha Adidas.
Golikipa
wa timu ya Taifa ya Italia Buffon
akiokoa penalti ya kwanza ya Uruguay iliyopigwa na Diego Forlan.
|
Kisha Buffon
akaokoa mikwaju ya Diego Forlan, Martin Caceres na Walter Gargano kuipa ushindi
Italia.
|
Nae Kipa
Gianluigi Buffon amekuwa shujaa wa Italia jana usiku(Juni 30,2013) baada ya
kuokoa michomo mitatu ya penalti na kuiwezesha The Azzurri kutwaa nafasi ya
tatu katika Kombe la Mabara baada ya kuifunga Uruguay kwa penalti 3-2.
Timu hizo
zilitoka sare ya 2-2 baada ya dakika 120 huku Italia wakitengeneza nafasi
nyingi zaidi za kufunga.
Davide
Astori aliwafungia Wataliano bao la kuongoza dakika ya 25 kabla ya Edinson
Cavani kusawazisha dakika ya 58.
Alessandro
Diamanti akaifungia bao la Italia dakika ya 73, kabla ya Cavani kusawazisha
tena 78 na mchezo kuhakia katika muda wa nyongeza, ambako ilishuhudiwa Riccardo
Montolivo akitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya
njano.
Kisha Buffon
akaokoa mikwaju ya Diego Forlan, Martin Caceres na Walter Gargano kuipa ushindi
Italia.
Alberto
Aquilani, Cavani, Stephan El Shaarawy na Suarez wote walifunga kabla ya Mattia
De Sciglio kukosa.
Caceres
akakosa na Emanuele Giaccherini akafunga kabla ya Buffon kuokoa mkwaju wa
Gargano.
Washindi wa
tatu: Italia wakisherehekea kuifunga Uruguay huku Kikosi cha Italia kilikuwa:
Buffon, Maggio, Chiellini, Astori/Bonucci dk96, De Sciglio, Candreva, De
Rossi/Aquilani dk70, Montolivo, Diamanti/Giaccherini dk82, Gilardino na El
Shaarawy.
|
No comments:
Post a Comment