Basi la
kampuni ya Sumry limetumbukia mtoni Iku na kuuwa watu tisa na kujeruhi wengine Hamsini
na tatu Mkoani Katavi.
Ajali hiyo
imetokea katika kijiji cha Sitalike wilaya ya Mlele mkoani Katavi.
Tukio hilo
la kusikitisha lilitokea saa sita usiku kuamkia Julai 5, 2013 ambapo Basi hilo
lilipokuwa likitokea mjini Sumbawanga kuelekea Mjini Mpanda mkoani Katavi likiwa na abiri
waliokuwa wametoka Mkoani Mbeya.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Katavi Emanuely Nnley alisema jana kuwa ajali hiyo ilihusisha basi
aina ya Nissan Diesel lenye namba T909 AZT mali ya Kampuni ya Sumry lililokuwa
likiendesha na dereva aliyetajwa kwa jina na Stephano Chimane maarufu
kwa jina la Ntungu.
Alisema basi
hilo lilipofika katika daraja hilo lenye kona kali na mteremko dereva wake
alishindwa kulimudu na kulenga daraja hali iliyosababisha tairi za nyuma
kupanda juu ya ukingo na kutumbukia mtoni ambapo dereva wa basi hilo aliweza
kutoka na kukimbilia kusikojulikana .
Mkuu wa mkoa
wa Katavi Dr Rajabu Rutengwe alitoa rambi rambi kwa wafiwa wote na kuwapa pole
wahanga wa ajali hiyo mbaya kutokea tangu mkoa huo uanze.
Habari kwa
Hisani ya http://lukwangule.blogspot.com
No comments:
Post a Comment