Kocha wa
Manchester United David Moyes leo hii amethibitisha kwamba mshambuliaji wa
klabu hiyo Wayne Rooney hayupo sokoni na ataendelea kuicheza klabu hiyo kwa
mingi ijayo. |
Akizungumza
kwenye mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu ajiunge na klabu
hiyo akichukua nafasi ya Sir Alex Ferguson, Moyes alisema: "Nimeongea na
Wayne Rooney.
Wayne yupo nyuma ya mabao 40 kumfikia Sir Bobby na Denis Law.
Wayne hauzwi - ni mchezaji wa Manchester United - na ataendelea kubakia kuwa
mchezaji wa Manchester United.
Nimekuwa na mikutano nae kadhaa. Amerudi kwenye
hali nzuri na anafanya vizuri mazoezini. Tunajaribu kufanya kila kitu kumrudisha
Wayne Rooney kuwa kama alivyokuwa zamani - Wayne Rooney ambaye tunamjua.
Ronaldo na Rooney. |
"Vyovyote
vilivyotokea kabla, tunafanya kazi pamoja sasa. Macho yake yanaonyesha ni mtu
mwenye furaha, ni lazima niseme Wayne hauzwi. Kuliwahi kuwepo mkutano wa siri
baina ya Rooney na Sir Alex. Mie naendelea mbele sasa, sijui nini kilizungumzwa
kwenye mkutano huo. Ninachofikiria sasa ni kusonga mbele na kufanya kazi ya
kumrudisha Wayne Rooney kwenye ubora wake. "
Alipoulizwa
kuhusu Cristiano Ronaldo, Moyes alijibu: "Sitomzungumzia yeye moja kwa
moja na wachezaji wengine wa vilabu vingine. Lakini hii klabu siku zote imekuwa
ikivutiwa na wachezaji bora duniani."
Pia Moyes
alithibitisha kwamba winga mpya wa klabu hiyo aliyesajiliwa kutoka Crystal
Palace - Wilfred Zaha ambaye amekuwa akiwindwa na vilabu vingi kujiunga navyo
kwa mkopo - Moyes amesema mchezaji huyo ataungana na Manchester United kwenye
tour ya pre-season, kama ilivyo kwa wachezaji wengine.
Wakati huo
huo alipoulizwa kuhusu usajili wa wachezaji wapya, Moyes amesema angependa
kusajili wachezaji mapema lakini mambo yamekuwa yakichelewa kutokana na makocha
ambao ndio wanaothibitisha uuzwaji wa wachezaji wengi wamekuwa likizo au ndio
wanaingia kwenye vilabu vyao vipya.
No comments:
Post a Comment