Aidha Mashindano
ya Ngoma za Asili kanda ya ziwa kwa Mwaka 2013 yanadhaminiwa na BALIMI EXTRA
LAGER kwa mwaka wa nane sasa.
Madhumuni ya
mashindano haya ni Kufurahi pamoja na
wakazi wa maeneo ya Kanda ya ziwa na Wanywaji wa BALIMI katika kipindi hiki cha
sherehe za Mavuno,Kuenzi na Kulinda tamaduni zetu zisipotee na Kukutanisha watu,Kufahamiana na Kufurahi
pamoja ili Kulinda Amani na Upendo wa Nchi.
Mashindano
yaliyosalia ni Mkoa wa Mwanza ,Jumamosi ya Julai 06,2013 kwenye uwanja wa CCM
Kirumba,Mkoa wa Mara,Jumamosi ya Julai 13,2013 kwenye Bwalo la Magereza huku
Mashindano ya Kanda yakitaraji kufanyika
Jumamosi ya Julai 20,2013 katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.
Mshindi
katika Ngazi ya MKOA ataondoka na Zawadi ya FEDHA ambapo:-
1.Mshindi wa
Kwanza shilingi 600,000.
2.Mshindi wa
Pili shilingi 500,000.
3.Mshindi wa
Tatu shilingi 400,000.
4.Mshindi wa
Nne shilingi 300,000.
5.Mshindi wa
Tano hadi wa Kumi kila kikundi shilingi 150,000.
Mshindi
katika Ngazi ya KANDA ataondoka na
Zawadi ya FEDHA ambapo:-
1.Mshindi wa
Kwanza shilingi 1,1OO,000.
2.Mshindi wa
Pili shilingi 850,000.
3.Mshindi wa
Tatu shilingi 600,000.
4.Mshindi wa
Nne shilingi 500,000.
5.Mshindi wa
Tano hadi wa Kumi kila kikundi shilingi 250,000.
No comments:
Post a Comment