Tuzo za Muzizki Tanzania maarufu kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013, Kala Jeremiah na tuzo 3 huku Lady Jaydee na Diamond wakiibuka Wasanii Bora. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, June 09, 2013

Tuzo za Muzizki Tanzania maarufu kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013, Kala Jeremiah na tuzo 3 huku Lady Jaydee na Diamond wakiibuka Wasanii Bora.


Kala Jeremiah akipokea tuzo zake za  Wimbo Bora wa Mwaka Hip Hop...... ni Dear God na Mtunzi Bora wa Mashairi Hip Hop na Msanii Bora wa Hip Hop.


Gardner G Habash akipokea tuzo ya Msanii Bora wa Kike kwa niaba ya Lady Jaydee.


Ommy Dimpoz kwa mara nyingine tena! Tuzo ya Video Bora ya Mwaka..Baadae..na Tuzo ya Wimbo Bora wa Bongo Pop wa Me and You.

Chalz Baba akiwa na Tuzo  yake ya Msanii Bora wa Kiume Band.


Mashujaa Band wakifurahia Tuzo ya Band Bora  na wimbo wa Risasi Kidole.


Ben Pol akiwa kwenye stage na tuzo yake ya Mtunzi Bora wa Mashahiri Bongo Fleva.


Usiku wa Tuzo za Muzizki Tanzania maarufu kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 umefanyika jana(Juni 08,2012).



Tofauti na miaka mingine ambayo tukio la utoaji tuzo tu ndio lilikuwa likionyeshwa kupitia kwenye TV pekee, na kuwanyima fursa Watanzania waishio nje ya nchi kufuatilia moja kwa moja, mwaka huu watumiaji wa mtandano wa Internet waliweza kuangalia tukio zima la utoaji wa Tuzo mwaka huu 2013 kwa Wasanii na Watayarishaji wanaendeleza Juhudi za Kuleta Maendeleo ya Tasnia ya Muziki nchini Tanzania.



Aidha unaweza sema 2013 Kimuziki  umekuwa mwaka mzuri zaidi  kwa msanii toka rock City Mwanza Kala Jeremiaha ambae  wimbo wake ‘Dear God’ umeweza kuchukua tuzo tatu katika Kilimanjaro Music Awards 2013.


Kala Jeremiah  amefanikiwa kunasa tuzo 3 muhimu mwaka huu, Dear God imeweza kumpa nafasi kubwa na kushinda tuzo katika kipengele cha wimbo bora wa Hip Hop.


Mwana FA.
Nguvu ya wimbo huo bila shaka ndiyo imemuwezesha pia kuondoka na tuzo ya msanii bora wa Hip Hop na Mtunzi bora wa mashairi ya Hip Hop.


Kala aliweza kuwapenya wasanii wazito kama Fid Q, Joh Makini, Mwana FA, Profesa Jay na mdogo wake katika game Stamina wa Moro Town waliokutana nae katika vipengele vya Hip Hop.


Wimbo huu ulitengenezwa na mtayarishaji chipukizi Dee Classic ambae pia alikuwa anawania tuzo katika kipengele cha mtayarishaji chipukizi wa Mwaka lakini hakuweza kushinda tuzo hiyo ambayo ilienda kwa Mesen Selector.


Msanii mwingine wa bongo fleva aliyeng’ara katika tuzo hizo ni Ommy Dimpoz ambae pia aliondoka na Tuzo tatu, ambazo ni Video bora ya wimbo bora ya mwaka, wimbo bora wa Bongo Pop ‘Me and You’ akiwa na Vannessa Mdee ambao pia uliwapa tuzo ya wimbo bora wa kushirikishwa/kushirikiana.
 


Washindi wa Tuzo za Muzizki Tanzania maarufu kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 ni pamoja na …:- 





Msanii Bora wa Kiume Bongo Fleva.....ni Diamond.




Msanii Bora wa Kike..... ni Lady Jaydee.




Video Bora ya Mwaka......ni Baadae ya Ommy Dimpoz.




Wimbo Bora wa Mwaka Hip Hop...... ni Dear God wa Kala Jeremiah.




Wimbo Bora Afrika Mashiriki..... ni Jose Chameleone na Valu Valu.




Wimbo Bora RnB...... ni Rama Dee na Kuwa na Subira.




Mtunzi Bora wa Mashairi Hip Hop na Msanii Bora wa Hip Hop...... ni Kala Jeremiah.




Wimbo Bora wa Mwaka Hip Hop...... ni Ney wa Mitego na wimbo wa Sema Nao.




Wimbo Bora wa Ragga/Dancehall......Dabo na wimbo wa Predator.




Rapa Bora wa Band......ni Fagasoni.




Msanii Bora wa Kiume Band....ni Chalz Baba.




Luiza Mbutu.
Msanii Bora wa Kike Band....ni Luiza Mbutu.




Mtayarishaji wa Wimbo Bora wa mwaka Band.....ni Amoroso.




Wimbo Bora wa Bendi......ni Mashujaa Band na wimbo wa Risasi Kidole.




Msanii Bora Anayechipukia ni.....Ali Nipashe.




Wimbo Bora wa Bongo Pop.......ni Ommy Dimples na Vanessa Mdee Me and You.




Msanii Bora wa Kike Bongo Fleva......ni Recho.




Mtayarishaji Bora wa Mwaka Bongo Fleva.....ni Man Water.




Mtunzi Bora wa Mashahiri ya Bongo Fleva......ni Ben Pol.




Wimbo Wenye Vionjo vya Asili.....ni Chocheeni Kuni wa Mrisho Mpoto.




Msanii Bora wa Kike Taarab....ni Isha Mashauzi.




Msanii Bora wa Kiume Taarab....ni Mzee Yusuf.




Mtayarishaji wa wimbo wa mwaka wa Taarab....ni Enrico.




Mtunzi Bora wa Mashahiri ya Taarab....ni Thabit Abdul.





Baada ya kushinda Tuzo Msanii Rama Dee akafunguka na kauli hii kwenye Akaunti yake ya Facebook.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad