![]() |
|
Mchezo wa
Wavu ama Volleyball , Ngara Volleyball ikawafunga wenyeji Ingo Nawe Seti 3-0
,Mchezo ukichezwa katika Uwanja wa Volleyball,Giteranyi nchini Burundi Juni 09,2013.
|
Timu ya
Walimu FC ilijikaza kiume na kulazimisha dakika 90 za mchezo wake na wanyeji
timu ya Ingo Nawe toka wilayani
Giteranyi nchini Burudni kumalizika kwa matokeo ya sare ya kufungana bao 2-2.
Mchezo huo
wa kirafiki wa Kimataifa uliofanyika Juni 09,2013, katika uwanja wa wilaya ya
Giteranyi na wenyeji-Ingo Nawe kutumia vema uwenyeji wao kuandika mabao 2
kipindi cha kwanza cha mchezo huo kupitia kwa wachezaji wao Samweli Eton a
Glasia Ntukamazina.
Kipindi cha
pili kilipoanza ,Walimu FC walibadilika na Kulinda heshima ya wilaya ya Ngara
kwa kupigana kiume kukomboa magoli hayo mawili yaliyofungwa na wachezaji wao
Mwl.Festo Chiwanga na Sevelin John.
Kocha wa
Ingo Nawe Nibaza Antoni licha ya Kufurahia mchezo huo wa kirafiki katika
kuboresha mahusiano mema ila uwanja kutokuwa na kiwango bora cha kuchezewa
ndicho kiliwaponza na kuruhusu kutoka sare.
Kwa upande
wake Faustin Malulu katibu Mkuu wa Klabu ya Walimu FC alisemaje kuwa Matokeo hayo ya sare yanatoa picha nzuri kwa Klabu yake hasa hivi
sasa ikiwa katika mkakati wa kujiboresha na kuomba Wadau kuisaidia kwa hali na
mali ili ifikie malengo ya kuwa tibu bora.
Katika
Matokeo ya Mchezo wa Wavu ama Volleyball
, Ngara Volleyball ikawafunga wenyeji Ingo Nawe Seti 3-0 na kumfanya Kocha wa timu ya mchezo huo ya Ingo
Nawe Joni Belikimas Mbogambi kukubali kipigo hicho bila kupepesa maneno kuwa
Ngara walijiandaa vya kutosha na kumudu kila idara zaidi yao.
Katika
mchezo wa Mpira wa Kikapu ama Basketball licha ya kukumbwa na utata wa maamuzi
kutoka kwa waamuzi wa mchezo huo Baby wa Ngara na Kleva wa Giteranyi,Wenyeji
Ingo Nawe wakatalwa na kuwafunga Ngara Vikapu 39 – 31.
Katika hatua
Nyingine mkuu wa mkoa wa Muyinga nchini Burundi Idefonsi Ntahunkunda amesema
kuwa ziara ya kimichezo waliyoifanya wilaya ya Ngara kupitia timu ya Walimu
FC imehamasisha ujirani mwema,amani na
ushirikiano katika wilaya yao ya Giteranyi na kwamba Serikali ya Mkoa wa
Muyinga itajipanga kuwasiliana na Serikali ya mkoa wa Kagera nchini Tanzania
kuona namna nzuri ya kuboresha ujirani mwema kupitia Michezo.















No comments:
Post a Comment