![]() |
|
Picha zikionesha
Ujenzi wa Kingo za Daraja Jipya la Rusumo ukiendelea ambalo ni Daraja la kimataifa
linalovuka Mto Kagera na kuunganisha nchi jirani za Rwanda na Tanzania.
|
Aidha Daraja
ni jengo lililoundwa kwa kusudi la kuwa na njia juu ya pengo au kizuizi.
Mfano
mzuri ni daraja linaloendeleza barabara juu ya mto au juu ya barabara nyingine.
Kuna aina
nyingi za madaraja. Ukubwa wa daraja unategemea upande mmoja upana wa kizuizi
kinachotakiwa kuvukiwa yaani upana wa mto na kwa upande mwingine uzito wa
mizigo itakayopita daraja.
Daraja la kuvukisha watu halina mzigo mkubwa
lakini daraja linalopokea njia ya reli au barabara kuu litabeba uzito mkubwa.
Kuna pia
madaraja yanayovusha mfereji juu ya mto hivyo kuwezesha meli kupita juu ya meli
nyingine.
Kwa jumla madaraja ni sehemu muhimu za
miundombinu wa kila nchi na hili la Rusumo linalounganisha nchi jirani za Tanzania na Rwanda ni mfano mzuri katika kuimarisha ujirani mwema ,Biashara na Utali pia.





















No comments:
Post a Comment