Morocco Jana(Juni
15,2013) waliipikua Tanzania Nafasi ya
Pili ya KUNDI C baada ya kuichapa Timu ya mkiani Gambia kwa Bao 2-0 katika
Mechi iliyochezwa huko Marrakech.
Bao za
Morocco zilifungwa na Barrada na Younes Belhanda.
Katika KUNDI
C, ambalo leo(Juni 16,2013) , Tanzania imeikaribisha Ivory Coast Jijini Dar es
Salaam, Ivory Coast ndio Vinara wakiwa na Pointi 13 baada ya Kuifunga Taifa
Starz bao 4 – 2,kwa magoli ya Traore mawili,Yaya Toure na Wilfreid, Morocco Pointi
8, Tanzania Pointi 6 na Gambia Pointi 1.
Ivory Coast
imefanikiwa kusonga hatua ya pili na ya mwisho katika kuwanai tiketi ya kucheza
Fainali za Kombe la Dunia na Kwa ushindi huo, Ivory Coast imetimiza pointi 13
ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote katika kundi hilo na sasa
itasubiri kucheza na mmoja wa washindi wengine wa makundi mengine tisa ili
kuwania kwenda Brazil mwakani.
Straika wa
Uganda, Emmanel Okwi Jana aliifungia Uganda Bao muhimu katika Mechi yao ya
KUNDI J la kuwania kwenda Brazil Mwaka 2014 kucheza Fainali za Kombe la Dunia
walipoifunga Angola Bao 2-1 na kutwaa uongozi wa Kundi hilo.
Katika Mechi
hiyo, Angola walitangulia kufunga kupitia Job lakini Uganda walipiga Bao 2
Wafungaji wakiwa Emmanuel Okw na Tonny Mawejje.
Ushindi huo
umewafanya Uganda wawe juu ya Senegal kwa Pointi 2 na leo huko Monrovia Lineria
itacheza na Senegal.
Kwenye KUNDI
E, waliokuwa Vinara, Congo wakiwa Nyumbani Pointe Noire, walijikuta wakipoteza
uongozi huo kwa kuchapwa Bao 1-0 na Burkina Faso kwa Bao la Aristide Bance na
sasa Burkina Faso wako kileleni Pointi 2 mbele ya Congo.
![]() |
|
Morocco 2
Gambia 0.
|
Burkina Faso
ndio walimaliza wa pili nyuma ya Mabingwa Nigeria kwenye AFCON 2013.
Katika Mechi
nyingine ya KUNDI E, Hetitriki ya Pierre-Emerick Aubameyang iliwapa ushindi wa
Bao 4-1 Gabon dhidi ya Niger na kuwa Pointi 2 nyuma ya Vinara Burkina Faso.
Wakiwa kwao,
Zambia jana walibanwa na kutoka Sare ya Bao 1-1 na Sudan ambayo haina matumaini
ya kusonga mbele.
Matokeo hayo
yamewafanya leo Ghana, ambao wako Ugenini kucheza na Lesotho, kuwa na nafasi
murua kutwaa uongozi wa KUNDI D ikiwa watashinda na kujiweka kwenye hali nzuri
kucheza na Zambia huko Accra katika Mechi yao ya mwisho ya Kundi.
RATIBA/MATOKEO:
[Kwenye
Mabano Matokeo Mechi ya kwanza]
Ijumaa Juni
14,2013.
Libya 2 Togo
0
Jumamosi
Juni 15,2013.
Botswana 3
Central African Republic 2
Zambia 1
Sudan 1
Uganda 2
Angola 1
Congo 0
Burkina Faso 1
Gabon 4
Niger 1
Cape Verde 1
Sierra Leone 0
Morocco 2
Gambia 0
Jumapili
Juni 16,2013.
16:00
Lesotho v Ghana [0-7]
16:00
Mozambique v Egypt [0-2]
16:00
Ethiopia v South Africa [1-1]
16:30 Rwanda
v Algeria [0-4]
17:30 Congo,
DR v Cameroon
19:00
Liberia v Senegal [1-3]
20:00 Guinea
v Zimbabwe [1-0]
20:00
Equatorial Guinea v Tunisia [1-3]
21:00 Mali v
Benin [0-1]










No comments:
Post a Comment