Rais Kikwete na viongozi mbalimbali wa nchi za
Afrika wakishiriki katika mijadala na vijana wa CPTM 29ers .
|
Viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika wakishiriki
katika mijadala na vijana wa CPTM 29ers .
|
Rais wa Sri Lanka akishiriki mjadala na vijana
wa CPTM 29ers.
|
Rais Omar Bongo katika mjadala huo.
|
Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Rais
Mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano katika mjadala.
|
Rais wa Nchi ya Sri Lanka na Dkt Mihaela Smith wakifuatilia
mjadala.
|
Rais Kikwete akipiga ngoma kuashiria mwisho wa
mjadala wa viongozi na vijana.
|
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete akisalimiana
na vijana hao.
|
Wageni mbalimbali katika mkutano huo.
|
Ujumbe wa Nchi ya Swaziland.
|
Ujumbe wa Nchi ya Tanzania.
|
Meza kuu.
|
Meza kuu.
|
Vijana nwa THT wakitumbuiza.
|
Viongozi mbalimbali.
|
THT wakitumbuiza.
|
Meza kuu wakifurahia onesho la THT.
|
Wanafunzi wakiimba kwa furaha.
|
Meza kuu wakishangilia.
|
Sehemu ya wageni(picha na Ikulu).
|
Rais wa
Tanzania Dk .Jakaya Kikwete amesema
wakati umefika kwa nchi za Afrika kubadilika kwa kuwekeza kwenye sayansi
na teknolojia kwa ajili ya kuboresha maisha ya watu wake na maendeleo endelevu
ya bara hilo.
Amesema changamoto kubwa inayoikabili Afrika ni ukosefu wa teknolojia ya Sayansi inayotoka nje ya bara hilo ambayo ni ghali kwa serikali na watu binafsi.
Dk. Kikwete alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano unaohusu Majadiliano ya Kimataifa kwa Manufaa ya Wote (ISPD) 2013, unaohudhuriwa na marais 9, marais wastaafu watano, wakuu wa serikali na wajumbe wapatao 800 kutoka nchi mbalimbali duniani.
Alisema Afrika haitaweza kupiga hatua katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii bila ya uwekezaji wa kutosha katika Sayansi na Teknolojia.
Alisisitiza kuwa uwekezaji huo ufanyike kwa vijana ambao mustakabali wa bara la Afrika unawategemea wao. Alisema mapinduzi ya Sayansi na Teknolojia ndiyo yatakayorahisisha huduma za kijamii katika nchi hizo.
“Tukiwekeza kwenye elimu ya Sayansi na Teknolojia tutasonga mbele katika maendeleo na kuinua uchumi wa nchi zetu kutokana na ubunifu watakaojifunza vijana wetu,” alisema.
Dk. Kikwete alisema nchi zinazoendelea zina changamoto kubwa ya kupambana na matatizo yao kutokakana na kukosa elimu ya Sayansi na Teknolojia.
Alisema upatikanaji wa teknolojia na ubunifu ndio njia pekee itakayozikomboa nchi hizo.
“Bidhaa nyingi za teknolojia zikipatikana, hazishikiki kutokana na gharama kubwa, lakini tukiwa na uwezo wa kuzitengeneza wenyewe, tutasonga mbele,” alisema na kuongeza kwa kuwataka viongozi hao kulijadili suala hilo katika mkutano huo.
Hata hivyo, Dk. Kikwete alisema nchi zote za Afrika zinapaswa kuanza elimu ya sayansi na teknolojia kwa watoto wao kuanzia shule za msingi.
Aidha, alizishauri nchi za Afrika kuanzisha vyuo vikuu na taasisi za utafiti wa Sayansi na Teknolojia kinyume chake mustakabali wa Afrika utakuwa shakani.
Marais wengine waliotarajiwa kuwasili kwenye mkutano huo ni pamoja na Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye hakuweza kufika baada ya kutoa udhuru.
No comments:
Post a Comment