Timu ya Taifa ya Hispania. |
Timu ya soka ya Taifa ya Hispania imeingia kwa mara ya kwanza katika
fainali ya michuano ya kombe la mabara inayoelekea ukingoni siku ya
Jumapili(Juni 30,2013) huko nchini
Brazil baada ya kuichapa Italia kwa mikwaju ya penalty 7-6.
Mabingwa hao
wa kombe la Dunia na kombe na Ulaya wamefaulu kuingia katika fainali hiyo baada ya kuishinda Italia kupitia mikwaju
ya penalti baada ya timu hizo kutowana jasho katika muda wa dakika tisini na
muda wa ziada wa dakika thalathini na kulazimika kutoana kwa matuta.
Mchezaji
pekee alieshindwa kuweka nyavuni bao la penalti ni Leonardo Bonucci na hivo
Jesus Navas wa Hispania kupachika bao la
ushindi.
Leonardo
Bonucci wa Italia akipiga mkwaju wake uliota mbawa na kuikosesha timu yake
kucheza Fainali ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara na Brazil.
|
Jesus Navas wa
Hispania alifunga Penati ya ya mwisho, chini anashangilia kwa kuilaza Italia
penati 7-6.
|
Fainali itapigwa
siku ya Jumapili baina ya Hispania na Brazil ambayo ilijikatia tiketi baada ya
kuichapa Uruguay mabao 2 -1 katika nusu fainali.
Brazil
imepewa nafasi kubwa ya kushinda michuano hiyo kwani watakuwa nyumbani chini ya mashabiki wao
katika uwanja wa Maracana.
Brazil ndio imelibeba
kombe hilo la mabara katika misimu miwili iliopita na pia ni Nchi pekee Duniani iliyotwaa Ubingwa wa Dunia
mara 5.
Hispania ambao
wameshakutana na Brazil mara 8 na kufungwa mara 4, kushinda 2 na sare 2, mara
ya mwisho kucheza Uwanja wa Maracana dhidi ya Brazil walifungwa Bao 6-1, ilikuwa
Mwaka 1950.
Neymar
Brazil.
|
Brazil
imepewa nafasi kubwa ya kushinda michuano hiyo kwani watakuwa nyumbani chini ya mashabiki wao
katika uwanja wa Maracana.
|
Baada ya
hapo mara nyingine tena kwa Hispania kucheza Nchini Brazil ilikuwa Mjini Salvador
na kufungwa Bao 1-0 Mwaka 1981 kwenye Mechi ya Kirafiki.
Katika Kombe
la Dunia, Brazil na Hispania zimecheza
mara 5 na Brazil kushinda 3 na Hispania kushinda mara 1 tu.
Katika Miaka
ya hivi karibuni, Hispania wamekuwa
wakicheza soka safi na la kuvutia sana
kwa Soka lao la staili yao ya ‘Tiki Taka’ ya kumiliki Mpira, pasi fupi na za
haraka.
Lakini
Brazil baada ya kusuasua, Mwezi Novemba
Mwaka Jana walimrudisha tena Luis Felipe Scolari, ‘Big Phil’, Kocha ambae
aliwapa Ubingwa wao wa mwisho wa Dunia Mwaka 2002, na sasa ‘Jongo Bonito’,
‘Gemu Nzuri’ au ‘Bomba, ’imefufuka tena.
KIHISTORIA
USO KWA USO:
JUMLA:
Mechi 8
USHINDI: Brazil 4 Spain 2
SARE: 2
MAGOLI
JUMLA: Brazil 11
Spain 8
Mechi
zenyewe:
FIFA
KOMBE LA DUNIA:
Jumla:
Mechi 5
USHINDI: Brazil 3 Spain 1
SARE: 1
MAGOLI
JUMLA: Brazil 10
Spain 5
1986
Spain 0 Brazil 1 [Guadalajara, Mexico]
1978
Brazil 0 Spain 0 [Mar Del Plata, Argentina]
1962
Brazil 2 Spain 1 [Vina Del Mar, Chile]
1950
Brazil 6 Spain 1 [Rio De Janeiro, Brazil]
1934
Spain 3 Brazil 1 [Genoa, Italy]
KIRAFIKI:
Jumla:
Mechi 3
USHINDI:
Brazil 1 Spain 1
SARE: 1
MAGOLI:
Spain 3 Brazil 1
1999
Spain 0 Brazil 0 [Vigo, Spain]
1990
Spain 3 Brazil 0 [Gijon, Spain]
1981
Brazil 1 Spain 0 [Salvador, Brazil]
Kocha Del Bosque. |
Chini ya Kocha
Del Bosque, Hispania ilitwaa Kombe la
Dunia Mwaka 2010 huko South Africa na Mwaka 2012 walitwaa Ubingwa wa Ulaya,
EURO 2012.
Kocha huyo Vicente del Bosque, pia yupo njiani kutwaa
Taji lake kubwa la tatu akiwa na Kikosi hicho lakini mwenyewe anaamini Brazil
ndio wenye nafasi kubwa ya kutwaa Kombe la Mabara.
Akiongea na
Wanahabari mara baada ya Mechi na Italy, Del Bosque alisema: “Brazil ndio wenye
nafasi kubwa. Wana Kombe la Dunia mara 5, Kombe la Mabara mara 3 na tunakutana
nao kwao Maracana, hii ni changamoto kubwa!”
No comments:
Post a Comment