![]() |
| Mh. Mnyika. |
a. UZITO WA KAULI YA LUKUVI.
Mwenyekiti Mbowe alizungumza jana, na wakati anaeleza ushahidi uliopo, na ushuhuda uliopo juu ya tukio hili, ameeleza vilevile kushangazwa na kauli za Waziri Lukuvi.
Kwa hiyo katika nukta hii,
tuongeze tu baadhi ya mambo ya msingi, ikizingatiwa kuwa waziri Lukuvi ni Waziri
wa Sera, Uratibu na Bunge.
Kauli yake, akiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, inamaanisha ni Ofisi ya Waziri Mkuu imezungumza Bungeni.
b. LUKUVI AMESEMA UONGO HUKU AKIJUA UKWELI.
Kauli ya Lukuvi inapaswa kubebwa kwa uzito mkubwa, na kwa kauli hiyo imedhihirika kwamba ni sera ya serikali kusema uongo, huku ikijua ukweli.
Kauli yake imedhihirisha kwamba, jambo hili la kutaka
kulidanganya Taifa, lina uratibu wa serikali kwa ujumla wake.
Kama Waziri wa
Uratibu katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu ndiye Mkuu wa shughuli za
serikali bungeni) anaweza kutoa uongo wa namna hiyo, maana yake kauli hizi
zimeratibiwa, na hivyo serikali bungeni imepoteza uhalali wa kimaadili (moral
authority) wa kuzungumza, kwa sababu imeratibu uongo wa moja kwa moja.
c. ASKARI WA FFU ALITUPA BOMU NA ALITOROSHWA NA ASKARI WENZAKE.
Kauli ya Waziri huyu iturudishe nyuma tu. Wakati anazungumza kwamba polisi walishindwakumkamata mhalifu kwa sababu eti wananchi wamechochewa muda mrefu na hivyo kulichukia jeshi la polisi kwa kiwangu cha polisi kushindwa kutekeleza wajibu wake wa kumkamata mhalifu, wakati ukweli wa mikanda tuliyo nayo unaonyesha kuwa polisi ndio ambao waliamua kumtorosha mhalifu.
Sio tu kumtorosha kwa magari, bali kwa matumizi ya bunduki na bastola kuwapiga risasi wananchi waliokuwa wanafanya ulinzi shirikishi wa kuelekea kumkamata mhalifu waliyemwona, kwa sababu tu mhalifu huyo amevaa mavazi ya FFU, kwa sababu tu mhalifu huyo ni mwenzao.
Polisi hawa wakatekeleza uhalifu mwingine wa kupiga raia risasi ili kulinda uhalifu.
Jeshi la namna hii haliwezi kutetewa.
d. WANAOWATUMIA POLISI VIBAYA NDIO WANAWATETEA POLISI.
Watetezi pekee wa jeshi la namna hii ni watu kama Waziri Lukuvi, ambaye
Kama ambavyo alimtetea Kamuhanda kwa mauaji ya Daudi Mwangosi kwa kupigwa na bomu tumboni, ndivyo ambavyo Lukuvi amesimama bungeni kutetea askari aliyeua raia kwa bomu, askari walioua raia kwa risasi ni mwendelezo wa serikali ya CCM kutetea mauaji. Ni ishara wazi kwamba mauaji ya namna hii yanayotetewa na serikali ni wazi yamepangwa na serikali.
e. SERIKALI, CCM WANAFANYA PROPAGANDA BADALA YA KUTOA NAFASI YA MAOMBOLEZO .
Sote tuna majonzi, sote tunaomboleza. Ni bahati mbaya kuwa serikali, CCM na bunge, badala ya kutoa nafasi kwa maombolezo, wakati ambapo hatujawazika wenzetu, wakati ambapo tuko katika kipindi cha maombolezo, wao badala ya kuomboleza wanafanya propaganda.
f. TAMKO HILI LINAKUJA SASA KUKANUSHA UONGO.
Tumelazimika kuzungumza jambo hili badala ya kuzungumzia majeruhi, ambao wapo hospitali na tunaendelea kuwahudumia mpaka sasa, badala ya kuzungumzia marehemu, ambao lewa wanapewa heshima, wengine watapewa heshima kesho, tumelazimika kuyazungumzia haya kwa sababu UONGO UKIACHIWA, UKASEMWA, UKASEMWA, UKASEMWA, watu wanaweza kuamini kwamba ni ukweli. Lakini ni wazi, UKWELI UKISEMWA WATU WACHACHE WANAWEZA KUDANGANYIKA KWA MUDA MFUPI SANA, LAKINI SIO WATU WOTE KWA WAKATI WOTE.
Watanzania tusikubali kudanganyika, kwa pamoja tuungane katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo, tuendelee kusimamia UKWELI, kuueleza UKWELI.
g. WAUAJI WAWAJIBISHWE.
Lakini baada ya kipindi hiki cha maombolezo kwa mauaji kama haya na mauaji mengine ambayo yametokea muda mrefu katika taifa letu, ni lazima tufike hatua tuseme hapa imetosha.
Ifike hatua tuseme,
waliohusika na mauaji haya, si tu yaliyotokea Arusha Juni 15 mwaka huu, bali
waliohusika na mauaji ya kuanzia yale ya Arusha Januari 5 2011, na mauaji
yaliyofuatia baada ya hapo: mauaji ya Igunga Mwezi Oktoba 2011 ya Marehemu
Mbwana Masoud, aliyekutwa ameuawa na kutupwa.
Mauaji yaliyofuata Arumeru,
alipochinjwa kiongozi wa Chadema Marehemu Mbwambo aliyechinjwa kwa msumeno, na
baadaye askari Polisi wakadiriki kumtorosha mtuhumiwa huyo mahakamani na mpaka
leo hajapatikana, na mauaji yote yaliyotokea baada ya hapo, ifike hatua tuseme
sasa imetosha.
Ifike hatua tuiwajibishe serikali, ambayo baada ya kushindwa kubaki madarakani kwa kuwatumikia wananchi, baada ya kushindwa kubaki madarakani hata kwa kutumia ufisadi na rushwa, kutoa rushwa kwenye chaguzi, lakini wananchi bado wanakubali mabadiliko.
Baada ya kushindwa
kung'ang'ania madarakani kwa siasa za UONGO, SIASA CHAFU ZA PROPAGANDA ZA
UDINI, UKABILA n.k., sasa wanafikiri kwamba wanaweza kung'ang'ania madarakani
kwa UMWAGAJI WA DAMU.
h. HAKUNA DOLA ILIYODUMU KWA KUMWAGA DAMU YA RAIA WAKE.
Historia ya dunia inaonesha kuwa hakuna dola iliyokataliwa na wananchi kwenye sanduku la kura, kwa nguvu ya umma, ikafanikiwa kubaki madarakani kwa kutumia askari, kwa kutumia umwagaji damu. Tanzania tunapita njia hiyo. Tusielekee huko.
i. CHADEMA TUTETEE AMANI HUKU TUKIDAI HAKI.
Sisi Chadema tunapenda amani ya nchi yetu, tutaendelea kutetea amani ya nchi yetu. Lakini hatutarudi nyuma katika kudai haki.
Haki za sisi tunaoishi, haki za waliokufa na haki za watakaokufa.
Hatutaacha, kwa sababu tukifanya hivyo itakuwa ni usaliti kwa imani kubwa
ambayo wananchi wameipa Chadema.






Kutokana na uvunjifu wa A mani unaoendelea kutendeka Tanzania hatuna bubi kusema kwamba;
ReplyDelete"Tanzania tuna Amani ila ni dhahiri kusema kwamba Tanzania tuna Utulivu tu"