PICHA:Kazi ya usalama wa abiria na kudhibiti Uzembe wa madereva kama hawa lipo mikononi mwa askari wa kikosi cha usalama barabarani nchini. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, June 19, 2013

PICHA:Kazi ya usalama wa abiria na kudhibiti Uzembe wa madereva kama hawa lipo mikononi mwa askari wa kikosi cha usalama barabarani nchini.


Hapa  basi  hilo la Kampuni ya  Hood lenye namba  T 751 AVL likinusurika   kugongana  uso kwa uso na basi la Sumry baada ya  kulazimisha  kulipita  lori katika eneo la mlima  Kitonga  huku kukiwa na  kona kali kiasi cha  basi hilo kutaka  kutumbukia katika korongo la mlima  huo kama  linavyoonekana kushoto ,kazi ya  usalama  wa abiria na kudhibiti  uzembe wa madereva kama  hawa katika mlima  Kitonga  lipo  mikononi mwa  askari wa kikosi cha usalama  barabarani mkoa wa Iringa ambao mwaka jana  waliagizwa na mkuu wa kikosi hicho Taifa  Mohamed Mpinga  kuweka askari eneo hilo  ila wameonyesha  kupuuzia.



Basi la kampuni ya  Hood lililokuwa  likitoka Tunduma  kwenda Dar es Salam likijaribu  kulipita lori  katika kona kali  za mlima  Kitonga.


Hapa  dereva  wa  basi hilo bila  kujali usalama  wa abiria  wake akiendelea  kutaka  kupenya jambo ambalo ni hatari  zaidi,akiwa katika harakati za  kulipita  Lori hilo.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad