![]() |
| Saida Karoli. |
Taarifa ya
Neville Meena imesema kuwa ingawa ni kweli kuna ajali ya boti iliyotokea,
mwanamuziki Saida karoli hakuwa mmoja wa waliokuwemo kwenye boti hiyo na yuko
hai.
Taarifa hiyo
imetoa angalizo kutafuta uhakika kwani inasemekana kuwa Saida Karoli ni mzima,
yupo jijini Dar es Salaam: “Nimetafuta namba yake ya simu sijaipata, ila
taarifa kutoka Bukoba na ofisi ya Ofisa Utamaduni Muleba zinasema siyo kweli…”
ameandika Meena.
Kuhusiana na
ajali ya boti, Meena amesema, “…ni kweli kwamba kuna boti imezama katika Ziwa
Victoria, na kulikuwa na uvumi mwingi mjini Bukoba na Wilayani Muleba kuhusu
mwanamuziki huyo kufariki lakini baadaye ikathibitika kwamba hakuwa mmoja wa
abiria.”
Aidha katika
taarifa za awali zilisema kwamba’’,…Mwanamuziki Saida Karoli amefariki baada ya kuzama kwenye maji kufuatia boti aliyokuwa akisafiri nayo toka Kisiwa cha
Goziba kuzama baada ya kukumbwa na
dhoruba na kuzama Ziwa Victoria.
Inaalifiwa
pamoja naye kuna watu wengine wamefariki dunia.






No comments:
Post a Comment