Real Madrid wamewafunga wakongwe wenzao wa Manchester United mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Old Trafford jijini Manchester. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, June 02, 2013

Real Madrid wamewafunga wakongwe wenzao wa Manchester United mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Old Trafford jijini Manchester.


Timu ya wachezaji wa zamani wa Real Madrid wamewafunga wakongwe wenzao wa Manchester United mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Old Trafford jijini Manchester, leo(Juni 02,2013).



Bao la Man United limefungwa na Van Nistelrooy katika dakika ya 67, wakati yale ya Madrid yamefungwa na Morientes dakika ya 40 na De La Red (84).




Kikosi cha United kilikuwa hivi: Van Der Gouw, Martin, Irwin, Johnsen, Stam, Van Nistelrooy, Scholes, Fortune, Blomqvist, Cole, Yorke



Rea Madrid: Sanchez, Pavon, Helguera, McManaman, Amavisca, Sanz, Hierro, Vazquez, Zidane, Morientes, De La Red.



Katika mechi hiyo pia, kocha wa zamani wa Man United, Alex Ferguson pia alikuwepo uwanjani ambapo alipata shangwe nyingi.


Dwight Yorke akipiga shuti pembeni ya Francisco Pavon.



Kocha Sir Alex Ferguson alikuwa jukwaani akishuhudia magwiji wa Old Trafford wakimenyana na magwiji wa Real Madrid katika mchezo wa kirafiki wa hisani.


Bryan Robson aliiongoza timu hiyo ya England mbele ya mashabiki zaidi ya 60,000 ikilala 2-1 kwa Real Madrid.





Picha ya pamoja ya magwiji wa Real Madrid na Manchester United


Sir Alex Ferguson na Sir Bobby Charlton.



Fernando Hierro na Denis Irwin walikuwa Manahodha katika mchezo huo ambao Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Fernando Morientes aliifungia bao la kwanza Real na Ruud van Nistelrooy, ambaye aliichezea kila timu kipindi kimoja, akaisawazishia United.


Sekunde kadhaa baada ya Dwight Yorke kugongesha mpira kwenye mwamba wa juu, Ruben de la Red akafunga bao la ushindi zikiwa zimesalia dakika tano.


Edwin van der Sar alikuwa bora alikuwa nyota wa mchezo kwa upande wa United kwa kuokoa michomo kadhaa ya hatari kabla ya kumpisha Raymond van der Gouw kipindi cha pili.


Magwiji wa Real Madrid wakimpongeza Fernando Morientes.


Ruud van Nistelrooy baada ya kuifungia United.


Edwin van der Sar aliokoa sana katika mchezo huo licha ya Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Fernando Morientes aliifungia bao la kwanza Real na Ruud van Nistelrooy, ambaye aliichezea kila timu kipindi kimoja, akaisawazishia United.



Claude Makelele akipambana na Paul huku Kipa Edwin van der Sar alikuwa bora alikuwa nyota wa mchezo kwa upande wa United kwa kuokoa michomo kadhaa ya hatari kabla ya kumpisha Raymond van der Gouw kipindi cha pili.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad