![]() |
Jose Mourinho. |
Klabu ya Chelsea imemteua tena Jose Mourinho kuwa
meneja wa klabu hiyo kwa Mkataba wa miaka minne na atarejea katika klabu ambayo
alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu ya England, Kombe la FA na mawili ya Kombe
la Ligi kati ya mwaka 2004 na 2007.
Mourinho
ambaye ni raia wa Ureno atachukua nafasi ya Kocha Rafael Banitez aliyejiunga na
Klabu ya Napoli ya Italia baada ya
kuinoa klabu hiyo kwa miezi sita.
Hii ni mara ya pili kwa Mourinho kurejea
Stamford Brigde kama kocha baada ya kuondoka miaka sita iliyopita.
Mourinho
ndiye alikuwa chaguo la kwanza la mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich baada
ya kuinunua klabu hiyo mwaka 2003 na ndiye kocha pekee kati ya tisa waliopita
klabuni hapo kuanzia kipindi hicho aliyeipa mafanikio zaidi.
Mourinho
ametua na benchi lake la ufundi linaloundwa na Rui Faria, Silvino Louro na Jose
Morais aliokuwa nao Real, ambao watafanya kazi pamoja na benchi la ufundi la
sasa la timu ya kwanza, Steve Holland, Christophe Lollichon na Chris
Jones,"ilisema taarifa ya Chelsea.
Bila shaka
Kocha Mourinho yu tayari kujipanga kuipa
Chelsea taji la kwanza la Ligi Kuu ya England msimu ujao tangu mwaka 2010.
Taarifa
katika tovuti ya klabu hiyo imesema: "Klabu ya soka ya Chelsea inayo
furaha kutangaza kuteuliwa kwa Jose Mourinho kama Kocha Mkuu wa kikosi cha
kwanza.
![]() |
Jose
Mourinho akiwa ameshika jezi ya Chelsea baada ya kuthibitishwa kocha mpya wa
Chelsea.
|
No comments:
Post a Comment