![]() |
| Mabingwa Manchester United. |
Ratiba ya Ligi Kuu soka nchini
Uingereza imetoka leo(Juni 19,2013) na
mechi ya kwanza ya David Moyes nyumbani kama kocha mpya wa Manchester United
itakuwa dhidi ya Cheslea yenye kocha mpya pia, Kocha Jose Mourinho.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu, Manchester United watakuwa na mwanzo mgumu katika ligi
hiyo msimu ujao 2013-14 wakisafiri kuwafuata Liverpool na Manchester City ndani
ya mechi tano za mwanzoni.
Mechi ya kwanza kwa Meneja mpya wa Manchester City,Kocha Manuel Pellegrini, ni Nyumbani Uwanja wa
Etihad kwa kucheza na Newcastle.
![]() |
| Kocha David Moye. |
Manchester United itaanza na
mabingwa wa Kombe la Ligi, Swansea Agosti 17, kabla ya kurejea nyumbani
kumenyana na Mourinho na Chelsea yake Old Trafford wikiendi inayofuata.
Mechi na Liverpool itafuatia Agosti 31 kabla Dabi ya kwanza ya Jiji la Manchester itachezwa
hapo Septemba 21 Uwanja wa Etihad kati Manchester City na Manchester United na Marudiano ni Old Trafford Machi 1.
Arsenal wataanza Msimu wao wakiwa Nyumbani Emirates kwa kucheza na
Aston Villa huku Liverpool pia wakiwa Nyumbani kuivaa Stoke City na Tottenham
wataanza Ugenini dhidi ya Timu iliyopanda Daraja Crystal Palace.
![]() |
|
Zilizopanda:Hull
(Picha Juu ) na Cardiff (picha chini) zote zitacheza nyumbani mechi za kufunga msimu wa
Ligi kuu Uingereza 2013/2014.
|
MECHI ZA UFUNGUZI LIGI KUU ENGLAND 2013/2014 ni (AGOSTI
17,2013).
Arsenal v Aston Villa
Chelsea v Hull City
Crystal Palace v Tottenham Hotspur
Liverpool v Stoke City
Manchester City v Newcastle United
Norwich City v Everton
Sunderland v Fulham
Swansea City v Manchester United
West Bromwich Albion v Southampton
West Ham United v Cardiff City









No comments:
Post a Comment