Mungu amrehemu,Marehemu Albert Mangweha azikwa kishujaa kwenye makaburi ya Kihonda mkoani Morogoro. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, June 06, 2013

Mungu amrehemu,Marehemu Albert Mangweha azikwa kishujaa kwenye makaburi ya Kihonda mkoani Morogoro.


Hapa ndipo Mwili wa Marehemu Albert Mangwea ulipopumzishwa leo (Juni 06,2013) Mkoani Morogoro.



Baada ya siku kadhaa zilizokuwa na kila aina ya harakati, ugumu na majonzi makubwa, Albert Mangweha aka Ngwair hatimaye leo amezikwa kwenye makaburi ya Kihonda mkoani Morogoro ambako ni nyumbani kwao.



Kabla ya kuzikwa, wananchi wa Mkoa wa  Morogoro walipata fursa ya kuuaga mwili wake kwenye uwanja wa Jamhuri.



Umati mkubwa wa wananchi ulijitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Ngwair aliyefariki nchini Afrika Kusini, wiki iliyopita.



 Wasanii wengi kutoka Dar es Salaam nao wamehudhuria mazishi hayo.



Marehemu Albert Mangweha azikwa kishujaa sana ni umati usioelezeka mungu akulaze mahali pema peponi,” ameandika Izzo B kwenye Instagram.




Naye Lady Jaydee kupitia Twitter ameandika: Mpaka hapa tulipomsindikiza panatosha. Mungu amrehemu, kazi tumeimaliza. Life goes on.”



Marehemu Ngwear alizaliwa Novemba 16 mwaka 1982 huko Mbeya, huku asili yake ikiwa ni Mkoa wa Ruvuma akiwa mtoto wa mwisho katika familia yao.




Ngwea alitambulika katika sanaa ya muziki wa Bongo Fleva, hasa baada ya wimbo wake wa Ghetto Langu kupokewa kwa shangwe na mashabiki wake, akitoa nyimbo nyingine nzuri, kama vile Mikasi, Mimi, She Got a Gwan, Speed 120, CNN na nyinginezo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad