![]() |
Said Salum
Afisa Michezo wilaya ya Ngara anayeandika ,Afisa Taaluma wilaya Osward Rujuba wakifatilia
Michezo mbalimbali ya UMITASHUMTA ngazi ya Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.
|
![]() |
Vikombe na Vyeti vilitolewa kama ni zawadi kwa washindi wa Jumla Kiwilaya kwenye
Michezo hiyo ya UMITASHUMTA ngazi ya Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera.
|
![]() |
Huu ni muonekano wa Viwanja vya Michezo mbalimbali Vilivyopo katika shule ya Sekondari Kabanga wilayani Ngara Mkoa wa Kagera.
|
Kikosi cha
wanamichezo mbalimbali wapatao 78 kutoka
Halimashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera Kiko huko wilayani Muleba mkoani
Kagera ,kupambana kwa siku 3 katika Mashindano ya michezo mbalimbali kwa Shule
za Msingi nchini UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa wa Kagera ,mashindano yaliyoanza
Juni 05 hadi Juni 08 ,2013 katika Viwanja vya Michezo vya Chuo cha Ualimu
Katoke.
Akikiaga
kikosi hicho ,mkuu wa wilaya ya Ngara na mwenyekiti wa Michezo Costantine
Kanyasu licha ya kuwataka Vijana hao kudumisha nidhamu ya kiuchezaji wawapo
uwanjani pia wamewataka kuweka nia ya ushindi na mazoezi katika umri wao mdogo michezoni
ili kukuza vipaji vyao pamoja na kupata
mafanikio.
Kwa Upande
wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara Joni Shimilimana amewataka kupigana kwa dhati katika
mashindano hayo ili kuleta ushindi .
Nae mdau wa
michezo hapa wilayani na Mjumbe wa NEC taifa CCM Issa Husein Samma amesema
michezo ni ajira hivyo kuwataka vijana hao kujibidiisha na kujituma ili kupata
matunda mazuri kupitia Michezo.
Mashindano hayo ya michezo mbalimbali kwa shule za msingi
UMITASHUMTA ngazi ya mkoa wa Kagera yanashirikisha jumla ya wanafunzi zaidi ya
500 kutoka wilaya saba za Mkoa wa Kagera ambazo ni pamoja na Ngara,Bukoba,Manispaa,Karagwe,Biharamulo,Misenyi
na Muleba .
Kwa Mujibu
wa Afisa Michezo mkoa wa Kagera Kefa Eliasi amesema mashindano hayo ya UMITASHUMTA Ngazi ya mkoa
wa Kagera kwa mwaka huu yanashindanishwa katika Michezo ya Mpira wa
Miguu(Soka),Mpira wa Pete(Netball),Mpira wa Wavu (VolleyBall),Mpira wa Kikapu(Basketball),Riadha(mita 100,200,400,800,1500 na 3000),Handball,Mitupo
na Miluko.
No comments:
Post a Comment