NIGERIA 0
SPAIN 3.
|
Mashindano
ya FIFA ya Kombe la Mabara yanayochezwa huko Nchini Brazil leo (Juni 23,2013)
saa 4 usiku ,Kundi B limecheza Mechi zao za mwisho na Mabingwa wa Dunia
Hispania kuwachapa Mabingwa wa Africa Nigeria
Bao 3-0 na Uruguay kuibamiza Tahiti Bao 8-0.
Matokeo hayo
yamezifanya Hispania na Uruguay kuingia
Nusu Fainali ambako Hispania itacheza na
Italia na Uruguay kuwavaa Wenyeji wa Mashindano Brazil.
Katika Mchezo
wa Hispania na Nigeria,Bao za Jordi Alba, mbili, na Fernando Torres zimewapa Hispania
ushindi huo wa Bao 3-0 na hivyo kutinga Nusu Fainali kama Vinara wa
Kundi B ambapo watacheza Nusu Fainali na Timu ya Pili Kundi A ambayo ni Italia.
Nao Uruguay
wamefuzu kuingia Nusu Fainali baada ya kuifunga Tahiti Bao 8-0 na sasa
watakutana na Wenyeji Brazil.
Magoli ya
Uruguay yamefungwa na Abel Mathias
Hernandez Dakika ya 2, 24, 45 & 67 [Penati],Diego Perez 27,Nicolas Rodiero
62 na Luis Suarez 82 & 88.
Licha ya
ushindi huu, Uruguay hawakuacha ile asili yao ya utukutu baada ya Mchezaji wao
Andres Scotti Ponce de Leon kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu mara baada ya kukosa
kufunga Penati baada ya kupewa Kadi za Njano mbili.
Hata Tahiti
walimaliza Mtu 10 baada ya Teheivarii Wagemann kupewa Kadi za Njano mbili na
kutolewa kwa Kadi Nyekundu.
RATIBA
YA NUSU FAINALI
Jumanne Juni
26,2013.
[SAA 4
USIKU]
Neymar Brazil. |
Brazil v
Uruguay
Jumatano
Juni 27,2013.
[SAA 4
USIKU]
Spain v
Italy
MSHINDI WA
TATU
Jumapili
Juni 30,2013.
[SAA 1
USIKU]
FAINALI
Jumapili
Juni 30,2013.
[Rio De
Janeiro]
No comments:
Post a Comment