Pep Guardiola rasmi Kocha Mpya wa Bayern Munich akitambulishwa katika Mkutano na Waandishi wa Habari. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, June 24, 2013

Pep Guardiola rasmi Kocha Mpya wa Bayern Munich akitambulishwa katika Mkutano na Waandishi wa Habari.


Wanne mashuhuri: Guardiola aliungana na Matthias Sammer, Karl-Heinz Rummenigge na Uli Hoeness.


 Pep Guardiola anakuwa kocha wa mabingwa wapya wa Ulaya, Bayern Munich na tayari anajisikia nyumbani katikati ya watu.


Shinikizo? Pep Guardiola anakuwa kocha wa mabingwa wapya wa Ulaya, Bayern Munich.



Waliohudhuria mkutano huo wa kutambulishwa Guardiola bosi mpya Bayern.


Washindi  wa mataji matatu,Klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani wamemtambulisha kocha wao mpya, Pep Guardiola leo(Juni 24,2013) katika Mkutano na Waandishi wa Habari, The Bavarians wakijiandaa kuendelea kutamba katika soka ya nyumbani na Ulaya.




Kocha huyo wa zamani wa Barcelona amesema yuko tayari kukabiliana na changamoto za kufundisha timu iliyofanya vizuri msimu uliopita chini ya Jupp Heynckes, ikishinda mataji ya Ligi Kuu ya nyumbani na makombe mawili, pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya.




"Lazima nikubali mlinganisho," alisema Guardiola, akiwa katika vazi nadhifu la suti ya vipande vitatu ya rangi ya kijivu akizungumza Kijerumani kwenye Mkutano uliofanyika ukumbi wa mikutano wa klabu, Allianz Arena.




"Lazima niwe tayari kuishi na hiyo. Nipo chini ya shinikizo, wazi, lakini nafahamu hili na nakubali changamoto hii bila woga na ndiyo maana mimi ni kocha,"alisema.




Kocha Guardiola.
Guardiola, ambaye aliyeshinda mataji 14 katika miaka minne ya kuwa na Barcelona, usajili wake ni mkubwa Bayern na hasa ikizingatiwa anahamia timu iliyofanya vyema. Alitumia mwaka wake mzima baada ya kuacha kazi Hispania mwaka 2012, kwa kupumzika New York, Marekani.



"Kitu nachofikiria kwa sasa ni zawadi, baraka kuwa hapa na Bayern,"alisema kocha huyo Mspanyola, aliyesaini Mkataba wa miaka mitatu.




Aisema sababu ya kwanza iliyomfanya akubali ofa ya kuifundisha Bayern ni wachezaji wa klabu hiyo na historia yake.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad