![]() |
Hapa ndipo Mwili wa
Marehemu Albert Mangwea. |
Dawa za kulevya ni hatari, ni
hatari sana. Maisha ya baadhi ya wasanii na wachezaji yamepotea kutokana na
matumizi ya dawa hizo.
Aidha dawa za kulevya husababisha baadhi ya wasanii
na wachezaji kushindwa kuendelea na fani zao.
Orodha ya wasanii waliopoteza
maisha kutokana na matumizi ya dawa za kulevya ni ndefu lakini baadhi yao ni
Elvis Presley, Whitney Houston, Brenda Fassie wa Afrika Kusini.
Tanzania imepata mshtuko kwamba
kimeripotiwa kifo cha msanii kutokana na matumizi ya dawa za kulevya.
Tukiwa tunangoja ripoti kamili
ya daktari juu ya kifo chake, msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya ‘Bongo
Fleva’, Albert Mangwea ‘Mangwair au Ngwea’ anadaiwa kufariki kutokana na dawa
za kulevya nchini Afrika Kusini mapema wiki iliyopita.
![]() |
Hapa ndipo Mwili wa
Marehemu Albert Mangwea. |
Habari hizo ziwe kweli au la,
Mangwair amefariki na mwili wake ulirejeshwa nchini juzi kwa mazishi yaliyofanyika
leo hii(Juni 06,2013) huko Mkoani Morogoro.
Hata hivyo kifo chake, kitoe
changamoto kwa wasanii wengine akiwemo Ray C aliyeko kwenye kituo cha
kujirekebisha kutokana na matumizi ya dawa za kulevya.
DAWA ZA KULEVYA
Hizi ni dawa ambazo zimepigwa
marufuku kutumiwa na jamii kutokana na kiwango chake cha athari kwa binadamu.
Dawa hizi ambazo miongoni mwake
ni bangi, heroin na cocaine, zina athari zaidi katika mwili wa binadamu kuliko
faida.
Wasanii wanaotumia dawa za kulevya
husukumwa zaidi na tabia ya kuiga ili waweze kufanya maonyesho jukwaani kwa
ukakamavu mkubwa.
Wasanii hawa wanaamini
wanapotumia dawa hizo zinawasisimua mwili ili wapate uwezo wa kutumbuiza
jukwaani kwa muda mrefu bila kuchoka tena bila aibu.
Upande wa wanamichezo hasa soka
na riadha, msukumo mkubwa upo katika kuwa na pumzi ya kuweza kucheza soka kwa
dakika 90 bila kuchoka na moyo wa ujasiri hata kwenye riadha hali ni hivyo
hivyo.
ATHARI ZA DAWA ZA KULEVYA
MICHEZONI
Serikali duniani kote zinapiga
marufuku matumizi ya dawa za kulevya. Kwa bahati mbaya, dawa hizi hutengenezwa,
husafirishwa na hutumiwa kwa kificho japokuwa madhara hujionyesha wazi.
Kwa mujibu wa wataalam, mtu
anapotumia dawa za kulevya, moja kwa moja huathiri baadhi ya viungo vya mwili
kinyume cha imani ya watumiaji.
Mtumiaji hupata ganzi na kutoka
katika hali ya kawaida. Kutokana na ganzi hiyo taarifa hutumwa katika ubongo na
ubongo nao hutuma vichocheo katika kiungo hicho na hufanya kazi maradufu.
Jinsi dawa inavyotumiwa kwa
wingi ili kurekebisha hali ya ganzi ndivyo nguvu inavyozidi kutengenezwa na
hivyo ndivyo vinavyowamaliza wasanii na wanamichezo.
Wataalam wanasema matumizi haya
ya dawa za kulevya huufanya mwili wa mtumiaji kuchoka na kukosa hamu ya kula
kutokana na seli nyingi mwilini kushindwa kufanya kazi.
Matokeo yake, mwili wa mtu huyo
hudhoofu kwa kukosa chakula na hata uwezo wa kutengeneza chembechembe hai za
kuulinda mwili na kujikinga dhidi ya magonjwa hupungua, hivyo mwili huruhusu
magonjwa ya mara kwa mara.
Hali hii inapotokea uwezo wa
msanii au mwanamichezo huonekana umepungua na muda wowote mahala popote anaweza
kuchukua maamuzi anayoyajua yeye.
KITU CHA KUFANYA
Masomo ya dini za Kikristo na Kiislamu na elimu maalum ya dawa za kulevya
yatumike ili kuwaweka vijana katika misingi mizuri ya maadili na athari za dawa
za kulevya.
Hii itasaidia vijana kufahamu kwa undani faida za dawa zilizoidhinishwa
na Serikali na athari za dawa zilizopigwa marufuku zikiwemo za kulevya ili
kupunguza kwa wimbi la vijana kutumbukia katika matumizi ya dawa za kulevya.
MAKALA HII IMETOLEWA KATIKA GAZETI LA MAWIO NA IMEANDIKWA NA ELIUS
KAMBILI.
Hapa jeneza la Ngwair linaingizwa karubini, ikiwa ni picha inayoonyesha kuwa hatutaweza tena kukutana na msanii huyu hapa chini ya jua. R.I.P Ngwair.. |
Mbunge Sugu anamuaga Ngwair katika Uwanja wa
Jamhuri mjini Morogoro.
|
Hapa watu wanakanyagana kwa ajili
ya kujipanga mstari kwenda kumuaga marehemu Ngwair, leo katika Uwanja wa
Jamhuri mjini Morogoro.
|
Hapa M to The P akilia baada ya kupita
kwenye jeneza la Ngwair katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, kabla ya
mazishi yake yaliyofanyika Kihonda Kanisani jioni yake.
|
Uwanja wa
Jamhuri mjini Morogoro ulikuwa umejaa watu, sambamba na wale waliojipanga
barabarani kwa ajili ya kuangalia msafara wa Ngwair uliofunika mji wote siku ya
leo.
Tukio la
kuzikwa lilitanguliwa na shughuli ya uagaji iliyofanyika pia katika Uwanja wa
Jamhuri mjini Morogoro, baada ya kuona mkanyagano wa watu wengi nyumbani.
Makaburini
nako kulikuwa hakutoshi baada ya watu wengi kufurika, huku kila mmoja akiwa na
lake, wakiwapo wale waliokwenda kwa ajili ya kuangalia wasanii wao.
vijana wanapenda kuvamia mambo bila kujifunza kwanza kwa kuyafahamu na matokoe yake, wanatondokea kubaya!madaya ya kulevya ni hatari sana, ila ni mapema sana kudhani aliyekuwa komredi Ngwear amefariki kwa madawa ya kulevya.
ReplyDelete