![]() |
|
Wachezaji wa
Brazil wakishangilia ushindi wao kwa kuilaza Mexico mabao 2-0 bila ubishi na
sasa inatimiza ponti sita na kuzidi kujiimarisha kileleni mwa Kundi A.
|
![]() |
|
Nayman
akimtoka beki wa Mexico katika mchezo wa Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara
na Brazil kushinda bao 2-0.
|
Timu ya
taifa ya Brazil imeshinda mechi yake ya pili ya Kombe la Mabara, huku kijana
mdogo mwenye kipaji cha ajabu, Neymar akifunga bao tamu ndani ya dakika 10 za
kwanza kabla ya kumtengenezea nafasi ya kufunga bao la pili Jo.
Brazil
imeilaza Mexico mabao 2-0 bila ubishi na sasa inatimiza ponti sita na kuzidi
kujiimarisha kileleni mwa Kundi A.
Daniel Alves
alipinda krosi kutoka kulia na nyota mpya wa Barcelona, Neymar akaitokea wa
kwanza mbele ya beki wa Mexico, kabla ya kuhadaa na kumtungua kipa Jose Corona
dakika ya tisa na dakika ya 90 akampa pande Jo kufunga la pili.
Katika Mechi ya pili ya Kundi A la Mashindano ya
FIFA ya Kombe la Mabara ilichezwa kati ya Italy na Japan na kushuhudia piga
nikupige iliyomalizika kwa ushindi wa Italy wa Bao 4-3.
Matokeo hayo
yalihakikisha Wenyeji Brazil na Italy kuingia Nusu Fainali na Mexico na Japan
kutupwa nje ya Mashindano toka Kundi A.
Alhamisi
(Juni 20,2013) Usiku, Kundi B watacheza Mechi zao za pili na Mabingwa wa Dunia
Spain watacheza na Tahiti na kufuatia Mechi ya Mabingwa wa Afrika Nigeria dhidi
ya Uruguay.
Spain na
Nigeria zilishinda Mechi zao za kwanza kwa Spain 2 Uruguay 1 na Tahiti 1
Nigeria 6.











No comments:
Post a Comment