Meneja
wa Clouds media Group
Ruge
Mutahaba.
|
Uongozi wa Clouds
Media Group kupitia Mkurugenzi wake wa Utafiti na Matukio, Ruge Mutahaba
umemtaka msanii wa Bongo Fleva Judith Wambura 'Lady Jay Dee', ajipange na
kupokea changamoto badala ya kutafuta mahali kwa kujiegemea kwa kueneza matusi
kwao.
Clouds Media
leo imefungua mdomo kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miezi mitano tangu Jay
Dee alipokuwa akiwarushia makombora kwa madai kuwa wameharibu soko la muziki wa
Bongo Fleva sambamba na kuitangaza bendi ya Skylight kwa ajili ya kuiangamiza
Machozi Bendi.
Akizungumza
muda mfupi uliopita katika kipindi cha Power Breakfast, Meneja wa Clouds Media
Group, Ruge Mutahaba ameelezea yafuatayo kuhusiana na tuhuma zilizotolewa na
msanii Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ wiki iliyopita:-
-Asema vita
ya Lady Jaydee ameielekeza sehemu isiyo sahii kama tatizo ni Bendi ya SkyLight
basi apambane kuipiku bendi hiyo na si kugombana na watu wengine
-Awaasa wasanii kukubali kupokezana vijiti na kujiandaa kwa maisha yajayo.
-Aelezea Clouds ilipomtoa Jaydee mpaka sasa alipo.
-Aaamua siku ya leo kutopigwa muziki wa Bongo Flava.
-Asema kuwa Clouds ni chombo binafsi kina maamuzi ya kufanya chochote pasipo kuvunja sheria.
-Asema siyo vizuri watu kuchafuana katika mitandao ya kijamii, kama kuna tatizo ni vyema kuonana na muhusika ili kumaliza tatizo.
-Awaasa wasanii kukabiliana na changamoto na si kuziona kuwa ni tatizo.
No comments:
Post a Comment