Kikosi cha timu ya Elimu Fc ambao ndiyo Mabingwa Bulaya Cup 2013.
|
Kikosi cha
Bunda Sport Club.
|
Mbunge
akisalimiana na Waamuzi wa Mchezo huo.
|
Mbunge
Esther Bulaya akikagua Timu ya Elimu FC kabla ya Mchezo.
|
Kombe
hiloooooooooooooooo
|
Picha zote
Na: Augustine Mgendi,Bunda.
|
Michuano ya
Kombe la Mbunge wa Viti Maalum Kupitia Vijana Mkoani Mara , Esther Bulaya
linalojulikana kama Esther Bulaya Cup
imemalizika wilayani Bunda Mkoani Mara ambapo Timu inayoundwa na
Wadau wa Elimu wilayani humo Elimu FC ikiibuka Bingwa wa Mashindano hayo kwa Mwaka
2013.
Michuano
hiyo ambayo ilikutanisha timu zaidi ya 30 kutoka wilayani Bunda ilimaliza
kwa kuzikutanisha timu za Bunda Sport Club na Elimu Fc, ambapo iliibuka bingwa
wa Kombe hilo kwa Mwaka 2013 kwa Mikwaju ya Penati 3-1 baada ya kufungana
bao 1-1 ndani ya dk 90 na kujinyakulia kitita cha Shilingi milioni moja pamoja
na Kombe.
Mshindi wa Pili
alipata zawadi ya Shilingi laki Tano huku mshindi wa tatu timu ya Town Star
ambayo iliifunga timu Majengo Fc bao 1-0 ilipata kiasi cha Shilingi laki 3 na
Seti ya Jezi ,ambapo baada fainal hizo Mbunge Esther Bulaya alikuwa na haya ya
kunena.
Akiongea
wakati wa kukabidhi Zawadi mbalimbali wa Washindi,Mbunge Esther Bulaya
alisema kuwa kuna baadhi ya watu ambao walikuwa wanapanga Mikakati
ya kuhujumu Mashindano hayo yasifanyike Mbunge ambapo alisema kuwa kufanya
hivyo ni kutowatendea haki Vijana wa Bunda ambao ndiyo walengwa wa Michuano
hiyo.
Mh Bulaya
aliahidi kuendelea kudhamini Michuano hiyo Mpaka Mwisho wa Ubunge wake na
kuongeza kuwa kama atafanikiwa tena kuwepo katika hiyo nafasi ataendelea
kufanya Michuano hiyo mpaka kufa kwake.
“Mimi
nashangaa sana kuna baadhi ya watu wanataka kuhujumu.
Mashindano
haya kitu ambacho hawatawatendea haki vijana wa Bunda maana ndiyo
walengwa,napenda kuwaahidi Vijana wenzangu nitaendelea kudhamini mpaka mwisho
wa ubunge wangu na kama nitaendelea kuwepo kwenye hii nafasi nitayadhamini
Mpaka kufa Kwangu”alisema Bulaya.
Aidha baadhi
ya Wadau wa Michezo wilayani humo walimpongeza Mbunge huyo na kusema kuwa
Michuano hiyo inajenga uzalendo wa Vijana wa Bunda huku wakimuomba kuiendeleza
Michezo hiyo kwani imeonyesha Mafanikio Makubwa tangu kuanzishwa kwake.
Walisema
wilaya ya Bunda ni mmoja ya wilaya Mkoani Mara ambayo iilikuwa nyuma katika
suala la Michezo lakini kwa Muda Mfupi sasa wilaya hiyo imeonekana kuwa kinala.
“Unajua
hii wilaya ilikuwa nyuma sana Kimichezo lakini tangu huyu Mbunge ameanzisha
haya Mashindano sasa hivi Bunda inaongoza kwa Michezo hasa Soka maana hata
bingwa wa Mkoa na Makamu wake wanatoka Bunda sasa hayo si Mafanikio”? alisema
Juma Mbano.
Michuano ya
Esther Bulaya Cup 2013 iliunganisha Michezo mbalimbali ikiwemo Michezo ya
bao,draft pamoja na Pool table,ambapo Michuano hiyo ni ya Tatu kufanyika na
kila Mwaka imekuwa na Mabadiliko Makubwa .
……….
Ulikuwa ni ubingwa wa Matuta…………….
|
Habari Na
Augustine Mgendi,Bunda.
No comments:
Post a Comment