![]() |
King Kibadeni. |
Klabu ya
Soka ya Simba imefikia Makubaliano na Abdallah Athumani Seif maarufu kama King
Kibadeni kuwa kocha mpya wa klabu hiyo
ya Simba ya Dar es Salaam .
Katibu wa
Simba SC, Evodius Mtawala sasa anaandaa Mkataba kulingana na makubaliano na
Kibadeni aliyekuwa kocha wa Kagera Sugar ya Bukoba msimu uliopita , kisha
ataupeleka kwa Kamati ya Utendaji ya klabu ukapitiwe tayari kwa gwiji huyo wa
Msimbazi kuusaini Jumatano.
Lakini
wakati taratibu za Mkataba zikiendelea, Kibadeni au Chifu Mputa ataanza kazi
kesho saa 1:00 asubuhi katika Uwanja wa Kinesi, Urafiki, Dar es Salaam.
Asubuhi ya
kesho, Kibadeni atawafanyia usajili wachezaji zaidi ya 40 wakiwemo kutoka nje
ya Tanzania ambao wanaomba kusajiliwa na mabingwa hao wa zamani wa Afrika
Mashariki na kati na Tanzania Bara.
Baada ya
usaili huo, wachezaji ambao watamvutia mfalme huyo wa mabao wa zamani nchini,
wataunganishwa na wachezaji waliosajiliwa Simba SC kwa ajili ya msimu ujao
kuanza rasmi maandalizi ya msimu mpya Jumatano, Uwanja wa Kinesi.
Mazoezi ya
Jumatano yatahusisha wachezaji wote, ambao hawapo katika timu zao za taifa,
yaani waliokuwepo kwenye kikosi cha msimu uliopita na wapya waliosajiliwa.
Wachezaji
ambao hawatahusika katika programu ya msimu mpya ya Simba SC ni Haruna Moshi
‘Boban’, Amir Maftah, Wilbert Mweta waliomaliza mikataba, Paul Ngalema,
Abdallah Juma walioomba kuondoka, Salim Kinje anayetolewa kwa mkopo, Juma
Nyosso na Ramadhan Chombo ‘Redondo’, ambao suala lao lipo kwa Kamati ya
Utendaji.
Katika
benchi la Ufundi, Kibadeni atakuwa anasaidiwa na walimu wawili, Mganda Moses
Basena na mzalendo Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, wakati Meneja atakuwa Nico Njohole
na mtunza vifaa atakuwa Ally Cheche.
Mtihani wa
kwanza wa Kibadeni unatarajiwa kuwa nchini Sudan mwishoni mwa mwezi ujao,
ambako Simba itacheza Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame
pamoja na wapinzani wao wa jadi, Yanga SC.
Simba SC
imepangwa Kundi A katika michuano hiyo pamoja na wenyeji El-Mereikh, Elman ya Somalia na APR ya Rwanda, wakati Yanga
ambao ni mabingwa watetezi, wamepangwa Kundi C na Ports ya Djibouti, Express ya
Uganda na Vital 'O' ya Burundi.
Katika
michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Juni 18 hadi Julai 2, mwaka huu mjini
Khartoum, Sudan, mabingwa wa Kenya, Tusker wamepangwa Kundi B pamoja na wenyeji
wengine, Al-Hilal, Falcons ya Zanzibar, Al Ahly Shandy ya Sudan na Al-Nasir
Juba ya Sudan Kusini.
Simba SC
itashuka dimbani Juni 21 kufungua dimba na El-Mereikh, wakati mabingwa
watetezi, Yanga wataanza kampeni zao za kutetea taji Juni 20 kwa kumenyana na
Express na mechi zote zitachezwa Elfashar.
WASIFU WA
KING KIBADEN.
19-Alizaliwa
mjini Dar es Salaam.
19-Alijiunga
na Simba SC akitokea.
1974-
Alifunga bao la kwanza katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Hearts Of Oak ya Ghana
nchini Ghana katika Robo Fainali ya Kwanza ya Klabu Bingwa Afrika.
1974-
Aliiongoza Simba kuwa rekodi ya kuwa klabu ya kwanza na pekee Tanzania kufika
Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika hadi sasa.
1978-
Alifunga mabao matatu peke yake katika ushindi wa 6-0 dhidi ya Yanga SC.
1993-
Aliiwezesha Simba SC kufika Fainali ya Kombe la CAF akiwa Kocha, rekodi ambayo
haijavunjwa hadi leo ikiwa ni miaka 20 baadaye.
19-Alistaafu
Simba SC na kwenda kuwa kocha Majimaji ya Songea.
No comments:
Post a Comment