Pumzika kwa Amani, Mbele yako, Nyuma yetu Albert Mangwea a.k.a Ngwair. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, May 28, 2013

Pumzika kwa Amani, Mbele yako, Nyuma yetu Albert Mangwea a.k.a Ngwair.



R.I.P Ngwair.
Msanii Maarufu wa Bongo Fleva Nchini Tanzania, Albert Mangwea Maarufu kama  Ngwair, amefariki dunia leo(May 28,2013) akiwa nchini Afrika Kusini.



Kwa mujibu wa Taarifa za Redio mbalimbali  jioni hii  nchini, inadaiwa Ngwair  amefariki dunia kutokana na matatizo ya matumizi ya dawa za kulevya. 



Kimuziki, Ngwair aliibukia  Mkoani  Dodoma ambako alikuwa katika kundi moja na Noorah pamoja na Mez B.



Baadaye akapata dili  Bongo Records  chini ya mmiliki wa studio hizo, Petter Matthysse ‘P Funk’ aliyemuinua zaidi kimuziki na kumfanya awe miongoni mwa wanamuziki nyota nchini.



Wimbo wake wa kwanza kutamba ni Gheto Langu mwaka 2003 ambao ulimpatia umaarufu kabla ya kutoa albamu yake ya kwanza a.k.a Mimi mwaka 2003 ambayo ilimpatia mafanikio makubwa na kubadili maisha yake.



Hata hivyo mafanikio hayo yalimlevya na kujitumbukiza kwenye utumiaji wa dawa za kulevya, hivyo kujikuta akishindwa kufanya kazi ya muziki kwa usanifu na kuanza taratibu kufilisika hadi kuuza mali zake zote, ikiwemo gari aina ya Jeep.



Ngwair kutoka kwenye kupanga nyumba nzima maeneo ya Sinza, Dar es Salaam akajikuta  anarejea kuishi katika ‘magheto’ ya washkaji zake sehemu mbalimbali Dar es Salaam.





Mwaka 2010, Athumani Tippo, mmiliki wa maduka ya Zizzou Fashions alijaribu kumuinua tena msanii huyo baada ya kumchukua kwenye lebo yake na kumuwezesha kutoa albamu ya pili, Nge.




Hata hivyo, Nge haikufanya vizuri sana na kuzidi kumchanganya msanii huyo hivyo kutopea kwenye dimbwi la utumiaji wa dawa za kulevya na ‘kuharibika zaidi’.  



Mafanikio yake zaidi ni kushinda tuzo ya Kilimanjaro Music Awards kama mwana Hip Hop Bora wa mwaka 2005. 



Mwaka 2003, msanii Wayne Wonder aliyekuja kutumbuiza kwenye Fiesta aliondoka na CD ya wimbo Mikasi ya Ngwair baada ya kuvutiwa na kibao hicho alichowashirikisha Mchizi Mox na Ferooz. 


 HII NDIYO HOSPITALI AMBAYO MWILI WA MANGWEA UMEHIFADHIWA..


Ngwea  amefariki  katika moja ya vitongoji vya jiji la Johannesburg na baadaye wenzake walimkimbiza katika Hospitali ya St Helen Joseph. 




“Baada ya kufika tuliambiwa ameshakufa, lakini imetushangaza sana,” alisema mmoja wa marafiki zake.


Lakini rafiki yake mwingine ambaye alikuwa mwenyeji wake, alisema Ngwea alikuwa katika hali nzuri tu.


Alikuwa aondoke leo kurejea nyumbani Tanzania, hivyo niliondoka nyumbani na kumuacha akiwa amelala. Lakini nikiwa njiani nilipigiwa simu kwamba alikuwa hajaamka na walikuwa wanampeleka hospitali.


Baadaye walinipigia simu kwamba alipoteza maisha tayari. Nilishangazwa sana, hadi sasa sijajua kwa kuwa cheti chenyewe kimeandikwa kizungu lakini unajua mwandiko wa madaktari,” alisema rafiki yake mwingine.


Lakini inaelezwa, Ngwea alirejea nyumbani akiwa anaonekana mchovu na kusema anataka kupumzika.


Siku iliyofuata alichelewa kuamka, hali ambayo iliwashtua wenzake baadaye kabisa.


Hospitali ya St Helen Joseph aliyolazwa iko katika barabara ya 1 Peth, Auckland Park jijini Johannesburg.



Ni moja ya hospitali kubwa lakini inayotibu watu mbalimbali wakiwemo wa kawaida, kwa nyumbani unaweza kuilinganisha na  Muhimbili.


2 comments:

Post Bottom Ad