Mokhamed
Khalfan akiwa na wanafunzi wake wa Chuo cha Sekhasa Mining Mjini Ngara.
|
Walimu wa Shule
za Msingi na Sekondari wilayani Ngara mkoani Kagera wakiwa katika maandamano ya Mei Mosi leo(May
01,2013)kuelekea uwanja wa Posta ya zamani mjini Ngara .
|
Afisa Elimu
Msingi wilayani Ngara Simon Mumbee akiwa na Afisa Elimu Sekondari Julius
Nestori wakielekea uwanja wa Posta ya Zamani tayari kwa maadhimisho ya siku ya
Wafanyakazi Duniani.
|
Afisa
Utamaduni na Micheza wilaya ya Ngara Said Salum akiwa katika kuburudisha maandamano ya May
Mosi wakielekea uwanja wa Posta ya Zamani tayari kwa maadhimisho HAYO ya siku ya
Wafanyakazi Duniani..
|
Wafunzi wa
Sekhasa Miningi na Wafanyakazi wa serikali za mitaa wilayani Ngara wakielekea uwanja wa Posta ya Zamani tayari kwa maadhimisho ya siku ya
Wafanyakazi Duniani.
|
Wanafunzi wa shule ya Msingi Ngara mjini wakiwa katika maandamano ya Mei Mosi 2013.Picha zote na Shabani Nasibu Ndyamukama. |
Katika Maadhimisho
hayo ya Siku ya Wafanyakazi Duniani pamoja na mambo mengine , Serikali imeombwa kutatua kero zinazowakabili
wafanyakazi nchini kwa kuboresha
mazingira ya kazi sambamba na Mishahara .
Katibu wa
TUCTA wilayani Ngara Bw Vedasto Nsinde
amesema serikali haina budi kupandisha mishahara kwa kima cha chini kuwa
Shilingi Laki tatu na elfu 15 kwa mwezi ili kwenda sambamba na upandaji wa gharama za Maisha ya sasa.
No comments:
Post a Comment